Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO Mzambia, Cletus Chama yuko huru kuanza kuichezea klabu yake mpya, Simba SC katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kesho baada ya Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kuwasili nchini.
Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba ITC ya Chama waliyemsajili kutka Dynamos ya kwao, Zambia imewasili na sasa anaweza kuanza kucheza.
Chama mwenye umri wa miaka 27 aliyewahi kuchezea pia Ittehad ya Misri, ZESCO United FC na Nchanga Rangers FC, zote za kwao pia, Zambia hakucheza mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi Simba ikiichapa 2-1 Mtibwa Sugar kwa sababu ya ITC.
Cletus Chama yuko huru kuanza kuichezea Simba SC katika Ligi Kuu baada ya ITC yake kuwasili nchini
Mbali na Chama, Manara amesema ITC ya kipa Deogratius Munishi ‘Dida nayo imewasili pia, hivyo naye anaruhusiwa kucheza pia.
Chama ni miongoni wachezaji nane wa kigeni, Simba SC baada ya mabeki Muivory Coast, Serge Wawa, Pascal na mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere, Waghana, beki Asante Kwasi, kiungo James Kotei na mshambuliaji Nicholas Gyan, Mganda Emmanuel Okwi na Mnyarwanda Haruna Niyonzima.
Ligi Kuu inatarajiwa kesho na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watafungua dimba na Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Na Simba SC itaingia kwenye mchezo huo ikitoka kushinda Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2LeuxFL
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms