• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2026 (49)
    • ►  Januari (49)
  • ►  2025 (318)
    • ►  Desember (70)
    • ►  November (4)
    • ►  September (1)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ▼  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ▼  Agustus (487)
      • KWA MWEZI MMOJA TU, WANAYANGA WAICHANGIA TIMU YAO ...
      • Scottsville Sunday 2 September 2018 Best Bets
      • Turffontein Saturday 1 September 2018 Best Bets
      • AKINA SAMATTA WAPEWA KUNDI JEPESI EUROPA LEAGUE…TI...
      • AMUNIKE AWASAMEHE WACHEZAJI SIMBA SC LAKINI AKATAA...
      • UCHAGUZI MKUU WA TASWA KUFANYIKA NOVEMBA 25
      • Predict and Win: MTN8 Semi-Finals Second Leg Promo...
      • Currie Cup 2018: Blue Bulls v Golden Lions Preview
      • UEFA Champions League Groups and Fixtures
      • UEFA KUANZISHA MASHINDANO YA TATU YA KLABU ULAYA
      • CHELSEA NA LIVERPOOL KUKUTANA RAUNDI YA TATU CARAB...
      • F1 2018: Italian Grand Prix Preview
      • WACHEZAJI WA YANGA WARIPOTI KAMBINI TAIFA STARS
      • SAMATTA AFUNGA TENA GENK IKIWAPA WAPINZANI 4-2 NYU...
      • LUCA MODRIC NDIYE MFALME MPYA WA SOKA ULAYA
      • RONALDO USO KWA USO NA MOURINHO MAN UNITED
      • SA Racing Preview - 31st August to 2nd September 2018
      • SOUTHGATE AMTEMA YOUNG, AMCHUKUA LUKE SHAW ENGLAND
      • Kenilworth Best Bets - Saturday 1 September 2018
      • ATHUMANI CHINA AUNGA MKONO AKINA KAPOMBE KUFUKUZWA...
      • Pro 14: Round 1 Preview
      • French Ligue 1: Week Four Preview
      • French Top 14 : Round 2 Preview
      • Currie Cup 2018: Pumas v Western Province Preview
      • WATCH: Gabuza Issues Apology to Orlando Pirates Fans
      • TIMU YA BANDA YAVUNA POINTI TANO KATIKA MECHI TANO...
      • GHARAMA ZA KUWAONDOA WACHEZAJI WA SIMBA TAIFA STAR...
      • YANGA SC NA RAYON SPORT KATIKA PICHA JANA NYAMIRAMBO
      • MIKONO SALAMA KULINDA LANGO LA BESIKTAS, LAKINI SI...
      • NIYONZIMA 'ALIPOJOUNGA TENA' NA YANGA SC LEO MJINI...
      • KUTINYU: USHIRIKIANO NDIYO SIRI YA MAFANIKIO NDANI...
      • KATIBU MKUU TFF, WILFRED KIDAU ALIPOZUNGUMZIA KUWA...
      • MTN8: Semi-finals Second Leg Preview
      • Italian Serie A: AC Milan vs Roma Preview
      • YANGA SC WAKAMAILISHA MECHI ZA MAKUNDI AFRIKA KWA ...
      • Aviva Premiership: Round 1 Preview
      • Mitre 10 Cup 2018: Round 3 Friday, Saturday & Sund...
      • Fairview Friday 31 August 2018 Best Bets
      • La Liga: Week Three Preview
      • R1 Million Soccer Season Promotion: Terms and Cond...
      • Italian Serie A: Week Three Preview
      • Vaal Thursday 30 August 2018 Best Bets
      • German Bundesliga: Week Two Preview
      • NFD: Week Three Preview
      • NYOTA SIMBA SC WAONDOLEWA TAIFA STARS KWA UTOVU WA...
      • Gabuza Walks off after Fan Abuse
      • English Premier League: Week Four Preview
      • Gabuza Walks off after Fan Abuse
      • PGA Tour: FedEx Cup Playoffs Preview
      • European Tour: Made in Denmark Preview
      • SCHWEINSTEIGER ANG'ARA BAYERN MUNICH IKISHINDA 4-0...
      • ETO'O AMSAIDIA GWIJI WA CAMEROON ALIYEPOTEZA FAMIL...
      • USHANGILIAJI WA MEDDIE KAGERE WAWAVUTIA MASHABIKI ...
      • BERAHINO AMALIZA UKAME WA MABAO WA SIKU 913
      • YANGA SC WAKIPASHA KIGALI LEO TAYARI KUIVAA RAYON ...
      • AKINA MSUVA WALAZIMISHA SARE NA MAZEMBE LUBUMBASHI...
      • Greyville Wednesday 29 August 2018 Best Bets
      • FIFA YAIRUHUSU SIMBA KUMTUMIA CHAMA, WAZAMBIA WAAM...
      • NRC 2018: Season Preview
      • India vs England: Fourth Test Preview
      • Bafan Squad to Face Libya
      • Mitre 10 Cup: Auckland v Waikato Preview
      • Mitre 10 Cup 2018: Counties Manukua v Taranaki Pre...
      • Watch: Manchester United v Tottenham Hotspur Highl...
      • Watch: Jose Mourinho Walks out of Press Conference
      • SIMBA SC NA MBEYA CITY KATIKA PICHA JANA TAIFA
      • AZAM FC NA NDANDA KATIKA PICHA JANA CHAMAZI
      • YANGA SC WAENDA KUCHEZA KIGOMA BAADA YA MIAKA 19…W...
      • SAMATTA: NILIUGULIA MAUMIVU BAADA YA KUUPIGA MGUU ...
      • MAHOJIANO YA BIN ZUBEIRY NA ABDUL MANENO 'DENIS LA...
      • AZAM FC 3-0 NDANDA FC (LIGI KUU TZ BARA)
      • SIMBA SC 2-0 MBEYA CITY (LIGI KUU TZ BARA)
      • ALLIANCE FC 1-1 AFRICAN LYON (LIGI KUU TZ BARA)
      • MTOTO WA SIMEONE AIFUNGIA BAO FIORENTINA MBELE YA ...
      • MAN UNITED 'CHA WOTE', YAGONGWA NA SPURS PIA 3-0 O...
      • AZAM FC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA NDANDA...
      • KAGERE AFUNGA MABAO MAWILI SIMBA SC YAIPIGA 2-0 MB...
      • MWINGINE TFF AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA K...
      • Exciting opening weekend of DPL action
      • Vaal Tuesday 28 August 2018 Best Bets
      • Hollywoodbets Murray Cup: And then there were two
      • RATIBA LIGI KUU YAPANGULIWA TENA, MECHI ZA AZAM, S...
      • 5 Talking Points: Rugby Championship
      • Opinion: 'Talent' is a four-letter word
      • SA Horse Racing Preview - 27th - 30th August 2018
      • MJUE PAUL RWECHUNFURA; KIPA WA ZAMANI PAMBA FC ANA...
      • SAMATTA MCHEZAJI BORA GENK AMKABIDHI JEZI SHABIKI ...
      • ATP Tour: US Open Ro128 Preview
      • WTA Tour: US Open Ro128 Preview
      • Dolphins Premier League 2018- 1st Weekend Results
      • YANGA SC KUIFUATA RAYON BILA MAKAPU, AMEFIWA NA MA...
      • PSL: Week Five Preview
      • Flamingo Park Monday 27 August 2018 Best Bets
      • BENZEMA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 4-1 LA ...
      • UGANDA 3-1 ETHIOPIA (CECAFA AFCON QUALIFIER)
      • STAND UNITED 1-2 MBAO FC (LIGI KUU TZ BARA)
      • SAMATTA AENDELEZA MOTO WA MABAO KRC GENK IKIPIGA M...
      • HAZARD AFUNGULIA MBWA CHELSEA YAICHAPA NEWCASTLE 2-1
      • UGANDA WAFALME WA SOKA YA VIJANA CECAFA, WAUNGANA ...
      • MTIBWA WAWAZIMA PRISONS 1-0 MANUNGU, MBAO FC WAIPI...
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE » KARIBU LIGI KUU YA 55, TUNATARAJIA UCHEZESHAJI WA HAKI ILI KUPATA BINGWA HALALI

KARIBU LIGI KUU YA 55, TUNATARAJIA UCHEZESHAJI WA HAKI ILI KUPATA BINGWA HALALI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BAADA ya miaka 16 ya kampuni ya simu ya Vodacom kuibeba Ligi Kuu ya Tanzania, hatimaye wameitupa na msimu huu hakutakuwa tena na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kama ilivyozoeleka.
Vodacom walioanza kudhamini Ligi Kuu mwaka 2002 wakiipokea Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yao ya Safari Lager, hawajaafikiana na TFF juu ya mkataba mpya na michuano inaanza leo.
Ni Benki ya Biashara ya Kenya (KBC) wameweka fedha kudhamini Ligi Kuu ambao wametoa dau dogo mno, kiasi cha Shilingi Milioni 420 kwa mwaka, ambayo haifikii hata nusu ya fedha zilizokuwa na Vodacom kwa mwaka.
Kwa udhamini wa KCB, kila timu itapata gawio la Sh. Milioni 15 kwa msimu mzima na ni kwamba Ligi Kuu itabebwa mno na fedha za haki za matangazo ya Televisheni kutoka kwa Azam TV ambao wanatoa gawio la Sh. Milioni 162 kwa kila timu kwa msimu.   
Mshambuliaji na Nahodha wa Simba SC, John Bocco akiruka dhidi ya wachezaji wa Kagera Sugar

Pamoja na yote, Ligi Kuu inarejea tena kwa mara ya 55 tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 kwa wigo finyu na hali dunia kabisa, ikishirikisha klabu za Dar es Salaam pekee.
Timu 20 zinatarajiwa kujitupa dimbani kuwania pointi za mwanzoni, katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi, unaoshikiliwa na Wana Jangwani, Yanga SC. 
Katika mechi za ufunguzi, Simba SC wakitoka kubeba Ngao ya Jamii kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Jumamosi iliyopita, leo wataikaribisha Tanzania Prisons kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Alliance FC na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Coastal Union na Lipuli FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na Kagera Sugar na Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, zote zikianza Saa 10:00.
Ligi hiyo itaendelea kesho na mabingwa wa kihistoria, Yanga SC watamenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru kuanzia Saa 12:00 jioni, JKT Tanzania watamenyana na KMC kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Dar es Salaam, Stand United wataikaribisha African Lyon kuanzia Saa 10:00 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Azam FC watamenyana na Mbeya City kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ikumbukwe msimu huu Ligi Kuu itakuwa na timu nne zaidi kutoka 16 za msimu uliopita, Bodi chini ya Mkurugenzi wake, Boniphace Wambura ikitambulisha mfumo mpya wa mashindano hayo.  
Historia ya Ligi hiyo inaanzia mwaka 1929 ilipoanzishwa kifukara, tu kwa sababu ya mapenzi ya watu na soka wakaamua kuungana na kuanzisha michuano ya kutafuta bingwa, ingawa ni timu za Dar es Salaam pekee zilizokuwa zikishiriki wakati huo.

Utawala wa Yanga umezimwa msimu uliopita baada ya kupokonywa taji na mahasimu wa, Simba SC

Kufika mwaka 1965, ilianzishwa michuano ya Klabu Bingwa Tanzania, ambayo ilikuwa inaanzia ngazi ya Wilaya, ikichezwa kwa mtindo wa mtoano, ingawa pia katika miaka miwili ya mwanzoni, timu za Dar es Salaam pekee ndizo zilizoshiriki.
Katika mfumo huo, bingwa wa kwanza ilikuwa ni klabu ya Sunderland ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ilifanikiwa kutetea ubingwa wake msimu uliofuata, kabla ya kuutema kwa Cosmopolitan ya Dar es Salaam pia mwaka 1967.
Lakini wakati wote huo, bado Tanzania ilikuwa haijawa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hivyo Sunderland hawakuwahi kucheza michuano ya Afrika. Cosmo ingekuwa ya kwanza kucheza Klabu Bingwa Afrika mwaka 1968 kama isingejitoa, lakini kwa kujitoa kwao, Yanga ilifungua historia ya ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye michuano ya Afrika mwaka 1969, baada ya kutwaa ubingwa wa nchi kwa mara ya kwanza mwaka 1968, kabla ya kuutetea mara nne mfululizo, katika miaka ya 1969, 1970, 1971 na 1972. Baada ya hapo, Sunderland ikiwa tayari imebadili jina na kuitwa Simba kurejesha taji lake mwaka 1973.
Simba ilishindwa kuutetea ubingwa wake msimu uliofuata mwaka 1974 baada ya kupokonywa na Yanga katika fainali ya kihistoria iliyofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza kwa kuchapwa mabao 2-1.  
Mwaka 1975 Yanga iliutema ubingwa huo kwa Mseto SC ya Morogoro, iliyoweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutoka nje ya Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa nchi.
Lakini Mseto ilishindwa kuteteqa taji hilo, ikapokonywa na Simba msimu uliofuata- na Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kutetea ubingwa huo kwa miaka mitano mfululizo, kuanzia mwaka 1976 hadi 1980.
Siri ya kutawala kwa Simba kwenye ligi hiyo kwa miaka yote hiyo ni kuyumba kwa Yanga baada ya kukumbwa na mgogoro mkubwa 1976, uliosababisha kukimbiwa na wachezaji wote nyota, hivyo kuanza upya kabisa kuunda timu. 
Ni ndani ya kipindi hicho Simba iliweza kulipa kisasi cha kuchapwa mabao 5-0 na Yanga mwaka 1968, wakati nayo ilipowatandika watani wao hao wa jadi 6-0 mwaka 1977.  
Juni 1, mwaka 1968 Yanga iliigaragaza Simba 5-0, mabao yake yakitiwa kimiani na Maulid Dilunga (sasa marehemu) katika dakika za 18 kwa njia ya penalti na 43, wakati mengine yalitiwa kimiani na Salehe Zimbwe dakika ya 54 na 89 kabla ya Kitwana Manara kupachika la kuhitimisha karamu ya mabao dakika ya 86.
Julai 19, mwaka 1977 Simba nayo ililipa kisasi kwa kuibugiza Yanga mabao 6-0, wafungaji wakiwa ni Abdallah 'King' Kibadeni aliyetikisa nyavu mara tatu katika dakika za 10, 42 na 89, wakati mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika za 60 na 73 na Selemani Sanga wa Yanga alijifunga dakika ya 20.
Kufika mwaka 1981, tayari Yanga ilikuwa imara tena na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ingawa msimu uliofuata iliutema kwa Pan African. 
Kuanzia mwaka 1982, mfumo wa Ligi ya Tanzania ulibadilishwa na kukawa na ligi tatu, kwanza ni Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza visiwani Zanzibar na Ligi Kuu ya Muungano.
Yaani baada ya kupatikana washindi wawili wa juu wa kila ligi, Bara na Visiwani, walikutana kwenye Ligi Kuu ya Muungano, kutafuta bingwa wa Tanzania na washindi wake.
Wakati huo, bingwa wa Ligi ya Muungano alikwenda kucheza Klabu Bingwa Afrika na mshindi wa pili alicheza Kombe la Washindi.
Baadaye timu ziliongezwa na kuwa tatu kila upande katika Ligi ya Muungano.
Mwaka 1983, Yanga ilirejesha taji hilo kwenye himaya yake, ingawa msimu uliofuata ililitema tena kwa Simba.  Kwa ujumla muongo mzima wa 1980, taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara lilikuwa la kukoponyana, kwani Simba nayo mwaka 1985 ilipokonywa taji hilo na Yanga, ambayo nayo ililitema kwa timu mpya katika Ligi Kuu msimu wa 1986, Tukuyu Stars ya Mbeya.
Tukuyu nayo iliwarejeshea Yanga taji lao mwaka 1987, wakati mwaka 1988 Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga ilijiingiza katika orodha ya timu zilizowahi kutwaa taji hilo. Mwaka 1989, Yanga ilifunga orodha ya mabingwa ya mabingwa wa muongo huo kwa kutwaa tena ubingwa wa Bara.
Simba iliibuka mwaka 1990 na kutwaa ubingwa huo, ikitoka kuponea chupuchupu kushuka daraja msimu uliopita. 
Kupokonyana taji kuliendelea hata kwenye muongo wa 1990, kwani Simba iliutema ubingwa huo kwa Yanga mwaka 1991.
Yanga iliutetea ubingwa huo mara mbili mfululizo katika miaka ya 1992 na 1993, kabla ya kupokonywa na Simba mwaka 1994. Simba ilifanikiwa kuutetea mara moja 1995.
Mwaka 1996 ndipo Ligi Kuu ya Tanzania Bara ilipozaliwa rasmi chini ya udhamini wa Bia ya Safari Lager, bia inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na ikijulikana kama Safari Lager Premier League, Yanga ndiyo iliyokuwa bingwa wake wa kwanza. Yanga iliutetea ubingwa huo kwa miaka miwili mfululizo 1997 na 1998. Mwaka 1999, Yanga ikiwa tayari imetwaa ubingwa kwa matokeo ya uwanjani, aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana na Michezo, Profesa Juma Athumani Kapuya, alitengua matokeo hayo kwa kuiongezea Mtibwa Sugar pointi za mezani, hivyo kuipiku Yanga. Hatimaye Mtibwa ilipata ubingwa wa mezani.
Mtibwa ilifanikiwa kutetea ubingwa mwaka 2000, kabla ya kupokonywa na Simba msimu uliofuata, 2001. Lakini Simba SC haikupata zawadi ya ubingwa kutokana na wadhamini TBL kujitoa baada ya kukasirishwa na idadi ya timu kuongezwa bila ya wao kushirikishwa.
Bahati nzuri Vodacom wakaichukua Ligi Kuu kuanzia msimu uliofuata, lakini Simba haikuweza kutetea taji hilo baada ya kupokonywa na mahasimu wao wa jadi, Yanga walioibuka mabingwa wa mwaka 2002.
Mwaka 2003 Simba iliyokuwa kali zaidi ilifanikiwa kuutwaa tena ubingwa huo na kuutetea mwaka 2004 kabla ya kupokonywa na Yanga 2005 ambao waliutetea 2006. Mwaka 2007, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilifanya mabadiliko ya kalenda yake, ikitaka Ligi yake iendane na ligi za Ulaya, hivyo ikaamua kuchezesha ligi ndogo ya mpito kumpata bingwa na mwakilishi wa Kombe la Shirikisho, kabla ya Ligi Kuu kuanza rasmi Agosti.
Simba iliibuka bingwa wa ligi hiyo, baada ya kuifunga Yanga kwenye fainali kwa mikwaju ya penalti 5-4, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kufuatia sare ya 1-1.
Lakini msimu uliofuata ikiwa chini ya Profesa wa Kiserbia, Dusan Savo Kondic, Yanga ilifanikiwa kuurejesha ubingwa wake msimu wa 2008 na kutetea msimu uliofuata ikiwa chini ya kocha huyo, ambaye hata hivyo msimu uliopita alitupiwa virago katia mzunguko wa kwanza tu wa ligi na nafasi yake kuchukuliwa na Mserbia mwenzake, Kostadin Bozidar Papic, ambaye alishindwa kubakisha taji Jangwani, baada ya Simba kuchukua kwa kishindo.
Simba ilishinda mechi zote ikiwemo mbili dhidi ya watani wa jadi, Yanga na kutoa sare mbili tu dhidi ya Kagera Sugar Bukoba na African Lyon Dar es Salaam, hivyo kutwaa ubingwa kwa mbwembwe za aina yake na kufanikiwa kuutetea 2010.
Mwaka 2011 Yanga SC walirejesha taji lao, kabla ya 2012 kulitema kwa Simba SC na huo ukawa mwaka wa mwisho kwa Wekundu wa Msimbazi kulitia mkononi taji la Ligi Kuu.
Katika kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2013, Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu mara nne hadi mwaka huu, ikilikosa mara moja tu, mwaka 2014 lilipochukuliwa na Azam FC.
Lakini utawala wao ukazimwa msimu uliopita, baada ya Wekundu wa Msimbazi kubeba taji la kwanza la Ligi Kuu tangu mwaka 2012.
Wakati Ligi Kuu ikizipoteza timu za Maji Maji na Njombe Mji FC zote za Nyanda za Juu Kusini mwa nchi zilizoshuka daraja msimu uliopita – msimu huu zimeibuka timu nyingine ambazo ni Coastal Union ya Tanga, Biashara United ya Mara, Alliance FC ya Mwanza, JKT Tanzania, African Lyon na KMC zote za Dar es Salaam.
Coastal, Lyon, JKT, Biashara iliyokuwa ikijulikana kama Polisi Mara zote zimewahi kucheza Ligi Kuu, wakati Alliamce FC na KMC zimepanda kwa mara ya kwanza kabisa. 
Pamoja na ongezeko la timu, TFF imerejesha mfumo wa timu mwenyeji kuchukua mapato yote ya mlanfoni huku pia timu zikiruhusiwa kusajili wachezaji 10 wa kigeni na kuwatumia wote kwa wakati mmoja.
Karibu msimu wa 55 wa Ligi Kuu. Tunatarajia ushindani zaidi, mchezo wa kiungwana na uchezeshaji wa haki ili kupata bingwa halali. 
Wachezaji wa Simba SC mwaka 1993 wakiingia uwanjani kwa ajili ya moja ya mechi zao za michuano ya Afrika

MABINGWA WA JUMLA LIGI KUU:
1965 : Sunderland (Dar es Salaam) 
1966 : Sunderland (Dar es Salaam) 
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam) 
1968 : Yanga 
1969 : Yanga 
1970 : Yanga 
1971 : Yanga 
1972 : Simba 
1973 : Simba 
1974 : Yanga 
1975 : Mseto SC (Morogoro) 
1976 : Simba 
1977 : Simba 
1978 : Simba 
1979 : Simba 
1980 : Simba 
1981 : Yanga 
1982 : Pan African 
1983 : Yanga 
1984 : Simba 
1985 : Yanga 
1986 : Tukuyu Stars (Mbeya) 
1987 : Yanga 
1988 : Coastal Union (Dar es Salaam) 
1989 : Yanga 
1990 : Simba  
1991 : Yanga 
1992 : Yanga 
1993 : Yanga 
1994 : Simba 
1995 : Simba 
1996 : Yanga 
1997 : Yanga 
1998 : Yanga 
1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro) 
2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro)  
2001 : Simba 
2002 : Yanga 
2003 : Simba 
2004 : Simba 
2005 : Yanga 
2006 : Yanga 
2007 : Simba (Ligi Ndogo) 
2008 : Yanga 
2009:  Yanga 
2010: Simba SC
2011: Yanga SC
2012: Simba SC
2013: Yanga SC
2014: Azam FC
2015; Yanga SC
2016: Yanga SC
2017: Yanga SC
2018: Simba SC


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Byqgh7 best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang KARIBU LIGI KUU YA 55, TUNATARAJIA UCHEZESHAJI WA HAKI ILI KUPATA BINGWA HALALI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2018/08/karibu-ligi-kuu-ya-55-tunatarajia.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 16.20
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MTANZANIA Alice Gyunda miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha taj...
  • BARCELONA 3-1 ALAVES
    BARCELONA 3-1 ALAVES
    from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2s2Iqyx
  • TUZO ZA LIGI KUU ZABORESHWA, SASA WACHEZAJI KUPEWA NA KING'AMUZI CHA AZAM TV
    Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura, akionyesha tuzo atakayokuwa akipewa Mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vod...
  • ARSENAL YAMUONGEZEA MSHAHARA SANCHEZ ASIENDE BAYERN MUNICH
    KLABU ya Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates. Ofa mp...
  • EPL: Week 36 Preview
    EPL: Week 36 Preview
    We preview week 36 of the 2017/18 English Premier League season which is set to get underway on Saturday 28 April.  We’re into the final s...
  • Woolavington 2000 - Final Field
    View the final field and betting for the Grade 1 Woolavington 2000 at Greyille this Saturday 3 June 2017. The final field for the Woolav...
  • NFD: Week 20 Preview
    NFD: Week 20 Preview
    This will be a tricky week in the GladAfrica Championship with some of the teams having the Nedbank Cup last 32 action in mind. However, I...
  • Cup Finals Weekend Preview
    We take a look at this weekend's big European Cup Final ties. Most of Europe’s big leagues are done and dusted but there’s still the...
  • CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    BAO pekee la beki wa kimataifa wa England, Ben Chilwell dakika ya 45 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford Uwanja wa...
  • YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    KLABU ya Yanga imewasimamisha wachezaji wake wawili, Dickson Ambundo na Mrundi Saido Ntibanzokiza kuelekea mechi ya Fainali ya Kombe la S...
Copyright Viral Sports: KARIBU LIGI KUU YA 55, TUNATARAJIA UCHEZESHAJI WA HAKI ILI KUPATA BINGWA HALALI