Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC Alfajiri ya leo imeondoka kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Mwadui FC.
Azam FC itakipiga na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui Ijumaa hii saa 8.00 mchana, ambapo baada ya mchezo huo itakuwa na kibarua kingine Musoma kuvaana na Biashara United Septemba 19 kabla ya kuelekea jijini Mwanza kumenyana na Alliance Septemba 23.
Msafara wa Azam FC utaondoka na wachezaji wote waliokuwa fiti kikosini, wakiwemo nyota saba waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa, nahodha Agrey Moris na msaidizi wake, Frank Domayo, David Mwantika, Mudathir Yahya, Yahya Zayed waliokuwa Taifa Stars.
Wengine wawili ni kiungo mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu (Zimbabwe) na Nickolas Wadada (Uganda).
Kuelekea mechi hizo tatu, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans van der Pluijm, amesema kuwa amekipanga kikosi chake kwa ajili ya ushindi huku akidai atakuwa na siku mbili za kukiweka sawa kikosi chake kabla ya kucheza Ijumaa.
“Kila wakati ni jambo muhimu kucheza kwa lengo moja la ushindi na timu inayoonyesha njaa kwa ajili ushindi itapata ushindi hiyo ni rahisi kwenye mpira, mpira unategemea na uamuzi (wachezaji), bila shaka unatakiwa kufunga bao moja zaidi ya mpinzani wako, hiyo inamaanisha kuwa wewe utashinda mechi hiyo,” alisema.
Akizungumzia kuwakosa awali wachezaji wake saba waliokuwa timu za Taifa yake kama kutamuathiri kuelekea mechi ijayo, alisema: “Mimi sidhani hivyo, walikuwa kwenye mazoezi nasi katika maandalizi ya mwanzo mwa ligi, wamecheza mechi ngumu sana za kufuzu hawajapoteza mechi zao, hii inamaanisha kuwa watarudi na matumaini wakiwa na morali nzuri sana cha muhimu wanatakiwa waonyeshe ari walizoonyesha kwenye mechi za Kimataifa.”
Azam FC inaelekea kwenye mechi hizo ikiwa imeanza vema ligi, kwa kushinda mechi zake mbili za awali ikizifunga Mbeya City (2-0) na Ndanda (3-0), na kujisanyia pointi sita zinazoifanya kukaa nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa nyuma ya Mbao iliyocheza mechi moja zaidi ikijikusanyia pointi saba.
Wakati huo huo: Azam FC imemtambulisha Makamu Mwenyekiti mpya, Omar Kuwe ambaye anachukua nafasi ya Abdulkarim Amin 'Popat' aliyehamishiwa kwenye nafasi ya Utendaji Mkuu wa klabu.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2x36ipj
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms