Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
KIPA Peter Manyika amesema kwamba Singida United imevunja mkataba naye baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu, hivyo amejiondoa rasmi na sasa ni mcheza huru.
Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Manyika amesema kwamba baada ya kushindwa kumpa stahiki zake nyingine za kimkataba, Singida United imeshindwa pia na kumlipa mishahara.
Amesema kwamba sababu hiyo amejiondoa kwenye timu anasubiri dirisha dogo aende kusaini timu nyingine aendelee na kazi.
Peter Manyika amesema amejiondoa rasmi Singida United baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu
“Wamenirudisha nyuma sana, mwanzo niliwaomba wanipe barua mapema ya kuniruhusu kuondoka, wao wakasema watalipa kila kitu nachodai kabla msimu haujaanza. Hadi sasa hivi hawajafanya chochote na wapo kimya,”
“Hivyo mkataba unasema kama hutaweza kumlipa mchezaji mishahara kwa miezi mitatu utakua umeuvunja. Hiyo miezi mitatu ilikwishapita, hilo ni moja kati ya mengi waliyoshindwa, hivyo dirisha dogo naweza kwenda popote ili nimalizie ligi,”amesema Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Manyika Peter aliyewika klabu ya Yanga.
Kwa sasa Manyika anafanya mazoezi kwenye kituo kinachosimamiwa na baba yake, Manyika ambaye pia ni kocha wa makipa wa timu za vijana za taifa.
Manyika mdogo alikuwa anauanza msimu wa pili Singida United baada ya kujiunga nayo kutoka Simba SC, klabu yake ya kwanza kabisa kwenye soka ya ushindani baada ya kuibukia shule na kuchaguliwa hadi timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2MPb9oH
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms