• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2025 (241)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ▼  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ▼  Agustus (411)
      • UK Racing Best Bets - Sunday 1 September
      • BARCELONA YABANWA, YATOA SARE YA 2-2 NA OSASUNA LA...
      • LIVERPOOL YASHINDA MECHI YA 13 MFULULIZO LIGI KUU ...
      • DULLAH MBABE ATWAA TAJI LA WBO BAADA YA KUMPIGA MC...
      • AGUERO AFUNGA MAWILI MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 4-0
      • TAMMY ABRAHAM APIGA MBILI LAKINI CHELSEA YALAZIMIS...
      • REFA AWANYIMA PENALTI MAN UNITED WATOA SARE 1-1 NA...
      • KABWILI NA ALLY NG’ANZI WAITWA KIKOSI CHA BARA CHI...
      • MO DEWJI AWATULIZA WANA SIMBA SC BAADA YA KUTOLEWA...
      • Fairview Best Bets Monday 2 September 2019
      • Hollywoodbets Greyville Best Bets - Sunday 01 Sept...
      • Turffontein Best Bets Saturday 31 August 2019
      • UK Racing Tips - Saturday 31 August 2019
      • Europa League Group Stage Draw
      • Player Profile: Pukki the ‘Finn’isher
      • International Racing: Sha Tin Best Bets Sunday 1 S...
      • Stand a chance to win a R500 SPAR voucher
      • Imali or Ibhokisi Terms and Conditions
      • International Rugby: Georgia v Scotland Preview
      • Aphiwe Dyanti B Sample Returns Positive for Banned...
      • French Top 14: Round 2 Preview
      • New Racing Markets: Racing Blitz and Daily Double
      • UEFA Champions League Awards and Reactions
      • Phaka Predictions - Currie Cup Semi Finals
      • Champions League Draw: Liverpool Grouped with Napoli
      • TAIFA STARS WALIVYOANZA KUJIFUA LEO BOKO VETERANI ...
      • SAMATTA APANGIWA LIVERPOOL, NAPOLI NA SALZBURG KUN...
      • VAN DIJK NDIYE MWANASKA BORA ULAYA, AWAANGUSHA MES...
      • JKT TANZANIA 1-3 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)
      • UK Racing Best Bets - Friday 30 August 2019
      • SIMBA SC YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAWACHAPA JKT TANZ...
      • Spring's the Thing!
      • EPL: Arsenal vs Tottenham Preview
      • MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DU...
      • Fairview Best Bets Friday 30 August 2019
      • ATP Tour 2019: US Open Preview (Round of 64)
      • WTA Tour 2019: US Open Preview (Round of 64)
      • SANCHEZ ATUA MILAN KUKAMILISHA UHAMISHO WA MKOPOPO
      • UK Racing Tips - Thursday 29 August 2019
      • JACKPOT KUBWA YA KIHISTORIA YA TANZANIA, SH MILION...
      • YANGA SC 0-1 RUVU SHOOTING (LIGI KUU YA TANZANIA B...
      • KMC 0-1 AZAM FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)
      • YANGA SC YAANZA VIBAYA LIGI KUU, YACHAPWA BAO 1-0 ...
      • EPL: Arsenal vs Tottenham Preview
      • German Bundesliga: Week 3 Preview
      • English Premier League: Gameweek 4 Preview
      • Italian Serie A: Week 2 Preview
      • MTN8: Semifinals 1st Leg Preview
      • Hollywoodbets Scottsville Polytrack - Results and ...
      • European Tour: Omega European Masters
      • NFD: Week Three Preview
      • Spanish La Liga: Gameweek Three Preview
      • Rugby World Cup: Top Try Scorer Tips
      • Rugby World Cup: Top Try Scorer Tips
      • Mitre 10 Cup: Round 4 Preview
      • MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA DOUGLAS MUHANI, MC...
      • All Blacks Announce Powerful World Cup Squad
      • Hollywoodbets Scottsville - Wednesday 28 August 20...
      • Currie Cup Semi-Final: Cheetahs v Sharks Preview
      • Rassie Made the Right Calls
      • SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA FUN...
      • AZAM FC YAANZA VYEMA LIGI KUU TANZANIA BARA, YAICH...
      • What We Learned from the past Weekend of Rugby Action
      • Springbok Player Profile: Siya Kolisi
      • WTA Tour: US Open Preview
      • ATP Tour: US Open Preview
      • Hollywoodbets Murray Cup 2019 - Semi-Final Results
      • 2019 KZN Racing Awards
      • UK Racing Best Bets - Wednesday 28 August 2019
      • WACHEZAJI 40 WAITWA KIKOSI CHA AWALI CHA TIMU YA T...
      • First T20I: Sri Lanka vs New Zealand
      • Second Test: West Indies vs India
      • Ravichandran Ashwin vs Quinton de Kock - the key c...
      • Durbanville Tuesday 27 August 2019 Best Bets
      • HONGERA YANGA SC KWA KUITOA ROLLERS, LAKINI ILI KU...
      • UK Racing Best Bets - Tuesday 27 August 2019
      • 31 Springboks Announced for the 2019 Rugby World C...
      • Team of the Week: EPL Round 3
      • GRIEZMANN APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA REAL 5-2 ...
      • Rugby World Cup News: Week 5
      • Brutal England Pound Ireland at Twickenham
      • Sharks hold off 14-Man Bulls to Qualify for Currie...
      • Flamingo Park Best Bets Monday 26 August 2019
      • UK Racing Tips - Monday 26 August 2019
      • KOVALEV AMDUNDA ANTHONY YARDE KWA KO RAUNDI YA 11 ...
      • AGUERO AFUNGA MABAO MAWILI MANCHESTER CITY YASHIND...
      • LIPULI YAANZA VYEMA LIGI, YACHAPA MTIBWA SUGAR 3-1...
      • SIMBA SC 1-1 UD SONGO (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)
      • SIMBA SC YAAMBULIA SARE 1-1 NYUMBANI NA UD SONGO N...
      • CHAMA, SHEKHAN NA MAREHEMU MUSSA MSANGI ENZI ZAO S...
      • Hollywoodbets Greyville Polytrack - Results and Re...
      • Rugby World Cup: Top Try Scorer Tips
      • Currie Cup 2019: Lions v Griquas Preview
      • MAHOJIANO MAALIM BIN ZUBEIRY NA ISSA MANOFU
      • AZAM FC 3-1 FASIL KENEMA (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)
      • KMC 1-2 AS KIGALI (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)
      • TOWNSHIP ROLLERS 0-1 YANGA SC (LIGI YA MABINGWA AF...
      • UK Racing Best Bets - Sunday 25 August 2019
      • SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAWABAMIZA ARSENAL 3-1...
      • CHELSEA YA LAMPARD YAZINDUKA ENGLAND, YASHINDA 3-2...
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ►  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE » SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA FUNDISHO

SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA FUNDISHO

Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
Imekuwa ni jambo la kushangaza huku wengi wakiwa hawaamini kilichotokea Kwani katika hali ya kawaida wadau wengi waliamini Simba ni lazima ipite hatua hii ya kwanza wakilinganisha na mafanikio ya msimu uliopita.
Yapo mengi sana yatasemwa kama ilivyo ada ila kwa upande wangu nimeona mambo yafuatayo na mengine nilishaandika katika makala zangu za siku za nyuma!
1. Usajili uliofanywa
Niliwahi kuandika nikishangaa na kuhoji kwanini klabu ya Simba inasajili wachezaji wengi zaidi ya 10 wakati tayari gari lilikuwa limewaka na kuhitaji kutia gia ya mwendo kasi..Kwani msimu uliopita walikuwa na kikosi bora ambacho kilikuwa na maelewano makubwa na kuwa na kasoro ndogondogo tu na pengine kuhitaji marekebisho madogo sana ili kuongeza uimara wao lakini cha ajabu ni sawa na kulizima gari ambalo tayari lilisha waka na kuanza kulisukuma tena.
Simba SC ya msimu uliopita ilikuwa na mapungufu yasiyozidi manne kwa maana beki wa kati mzoefu,kiungo mkabaji,winga mmoja wenye kasi na mshambuliaji mmoja wa kati aliyekamilika basi.Lakini cha kushangaza umefanyika usajili ambao hauendani na kile ambacho tulikisikia kikisemekana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari,unaposajili wachezaji zaidi ya 10 ni sawa na kuanza upya na kufanya kazi iwe ngumu kwa benchi la ufundi katika kutafuta muunganiko ukizingatia na mda wa maandalizi haukuwa wa kutosha hivyo kilichofanyika ni kurudi nyuma hatua tano huku ulishapiga hatua mbili mbele,na hapa ndipo ninapotamani kujua kama zile ripoti za mabenchi ya ufundi kila mwisho wa msimu huwa zinafanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili au ndio kufungana midomo kunachukua nafasi na walimu kubaki na siri nzito vifuani mwao?
2. Pengo la James Kotei na Emanuel Okwi bado linaonekana.
Siku niliyosikia James Kotei akijiunga na klabu ya Kaiza Chiefs ya huko Afrika Kusini nilishtuka sana ila nikajiuliza kwani tarehe za kufungwa dirisha la usajili bado?nikakuta muda bado upo nikasema kama Kotei kaachwa basi huenda Simba wamepanga kuleta kiungo wa kiwango cha juu katika ukabaji barani Afrika,siku zikapita mwisho nakuja kuona kuna kiungo kutoka nchini Brazil. Daah nilichoka nikawaza inawezekana vipi kwa timu ambayo imefikia katika hatua nzuri kuwa na kiwango bora kucheza kamali na wachezaji kutoka Bara lingine tena ambao sidhani kama walikuwa katika viwango bora huko walikotoka zaidi ya rekodi za kwenye Wikipedia? 
Nikajiuliza Simba imecheza na Nkana,AS Vita,Mazembe Kweli imeshindwa kuona kiungo wa haja ambaye ana kitu na kuleta tija ndani ya Simba SC? nikaenda mbali na kuwaza ni kweli Mkude anaweza kutimiza majukumu ya ukabaji?
Nani anaendelea kuwaaminisha kuwa Mkude ni kiungo mkabaji? ipo siku nitamchambua kwa kina  Mkude kwa nia njema kuonesha ubora na madhaifu yake ila kifupi ni kiungo mzuri kwenye kushambulia ila si mzuri kwenye ukabaji ndio mana uwepo wa Kotei ulileta muunganiko mzuri kwani Kotei alikuwa anakaba kwa kuzunguka eneo lote la kati huku mkude akikaba kwa kujimegea eneo jambo ambalo limewagharimu katika mechi ya UD Songo.
Pia usajili wa Kahata,na Deo Kanda bado hujaziba pengo la Okwi ingawa Deo Kanda anakasi na vitu vingi ila swala la kufunga na kutengeneza nafasi bado yupo nyuma kumlinganisha na Okwi labda tumpe muda ila kwa sasa bado.
3. Mtazamo wa mechi ya ugenini dhidi ya UD Songo uliwamaliza Simba SC.
Pamoja na kutolewa na UD Songo bado Simba SC wanakikosi kizuri kulinganisha na UD Songo na hata mafanikio na uzoefu bado Simba sc wapo juu,hivyo mtazamo wa kwenda kutafuta sare ugenini kwa timu kama UD Songo haukuwa sahihi kwani walikuwa na uwezo wa kushambulia na kupata matokeo ugenini ila mtazamo kuwa wapate hata sare ili waje kumaliza mechi Dar-es -salaam uliwamaliza na kujikuta wakiwa kwenye presha kubwa kwenye mechi ya marudiano lakini pia mwalimu aliendelea kufanya makosa kwa kutodhani kama UD Songo wanaweza kupata bao ugenini huku akijikita zaidi kushambulia lakini akisahau kuweka mbinu bora za ulinzi.
4. Benchi la ufundi lilitumia muda mwingi kuiandaa Simba bila kuwaza pia ubora wa UD Songo.
Kuna msemo unasema siku zote timu kubwa hujiandaa wao wenyewe bila kushughulika na timu ndogo wanazokutana nazo inaweza ikawa sawa ila pia lazima uangalie na aina ya michuano, Simba sc walikuwa kwenye mechi za mtoano ambapo kosa moja unatolewa lakini pia makosa ambayo waliyafanya kwenye mechi ya awali nilitegemea wangeyafanyia kazi kwani walifanya makosa zaidi ya matano ambayo kama UD Songo wangekuwa makini mambo yangekuwa tofauti lakini wakabaki na dhana ya wao ni timu kubwa na kujiandaa wakizingatia ubora wao na wakiamini wao ndio wenye haki ya kushambulia na kupata matokeo na pengine UD Songo hawatakiwi kupata bao bila kuwa na namna nzuri ya kuweka ulinzi.
Wakati Simba sc wakijivunia na ubora walio nao kwa upande wa UD Songo wao walijikita kuangalia ubora na udhaifu wa Simba sc na kweli waligundua mambo yafuatayo na kuyafanyia kazi.
●Simba wazuri kwenye kumiliki mpira ila hawana  kasi kwenye kushambulia hivyo njia nzuri ya kuwakabili ni kuwashambulia kwa kushtukiza na wakifanikiwa kupata mpira jambo la kwanza ni kurudi nyuma kwa haraka na kuziba mianya huku wao wakibaki kupiga pasi nyingi eneo la kati na kufanikiwa kuwadhibiti.
●Mipira ya krosi inapigwa na walinzi wa pembeni wakati mawinga wao wakiwa kati kuongeza idadi ya washambuliaji hivyo endapo utafanikiwa kuokoa mipira ya krosi ni vyema kuicheza pembeni na kuleta madhara makubwa kwa simba sc kwani pembeni kunakuwa kweupe sana uku mawinga wao wakiwa hawana nguvu katika ukabaji na kupelekea ukuta wao kutawanyika na kuwa na idadi ndogo ya walinzi uku wakiwa kwenye umbali mkubwa kati ya mlinzi mmoja kwenda kwa mlinzi mwingine
●Safu ya kiungo ya Simba sio wazuri kwenye kukaba wanapenda kuchezea mipira sana hivyo njia bora ni kuwa na wachezaji wengi eneo la kati na kutumia mipira mirefu kuwachosha viungo wa simba ambao hawapendi kukimbia kuutafuta mpira.
●Safu ya ulinzi ya Simba ina walinzi bora wenye uzoefu na umiliki mzuri wa mpira ila sio wepesi kwenye kugeuka na kufanya maamuzi ya haraka hivyo ukiwashambulia kwa kasi kwa kuwafuata ni rahisi kufanya makosa na kusababisha penalty au adhabu karibu na eneo la hatari kitu ambacho kilifanikiwa na kuwapatia bao UD songo kupitia kwa mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha wao Luis Jose Miquissone ambaye ndio alibeba mpango mkakati wa kuichachafya safu ya ulinzi ya Simba sc uku akipokea mipira kutoka pembeni na kuingia kwa kasi kwa kuwafuata walinzi wa kati.
●Ni vigumu kumiliki mpira mbele ya Simba hivyo jambo la kufanya ni kuwaacha wachezee mpira kwenye eneo lao hadi sehemu ya kati na kuanza kukaba kwa nguvu wakianza kusogea kwenye eneo la tatu la kiwanja  jambo litakalo pelekea kupoteza pasi zao na kupora mipira kwa urahisi.
● Kwa ujumla njia bora ya kuwadhibiti Simba ni kucheza mpira wa nguvu na kasi muda wote huku ukiwafikia kwenye miili yao kitu ambacho kitawachanganya na kuwatoa mchezoni na kuathiri  namna  ya uchezaji wao wa nipe nikupe.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo UD songo waliyagundua na kuyafanyia kazi ndio mana hata kwenye mahojiano mwalimu wao Chiquinho Conde aliweka bayana kwani waliingia wakijua nini  wanatakiwa kukifanya katika mchezo huo mgumu.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo yameiangusha Simba katika hatua za awali hivyo kuna haja ya kuwa makini kwenye usajili,chaguo la kikosi,jopo zuri la kusoma ubora na udhaifu wa timu pinzani na kutoa uzito sawa kwenye kila mchezo ulio mbele ili kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi.Kwa sasa si wakati wa kumtafuta mchawi yameshapita ni wakati wa kujipanga upya ili kurudi tena msimu ujao kwa nguvu na kasi.
(Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana kupitia Akaunti yake ya instagram @dominicksalamba au namba +255713942770)


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2UfvzaY best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA FUNDISHO. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2019/08/simba-sc-kutolewa-mapema-ligi-ya.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 14.21
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    VIUNGO, Muivory Coast Aubin Kramo Kouamé (kushoto) na José Luis Miquissone wa Msumbiji wakiwa kwenye mazoezi ya Simba leo Uwanja wa Mo Si...
  • Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Stand a chance to win your share of R100 000 cash! Play R5 or more using your Hollywoodbets account on the selected Lucky Numbers draws an...
  • Lucky Numbers Draw Times & Results
    Lucky Numbers Draw Times & Results
    All the information you need for the 501 Lotto draws offered by Hollywoodbets for Lucky Numbers and Powa Numbas betting! Get closing times...
  • PGA Tour: The Sony Open Preview
    We take a look at the Sony Open set to take place between 11 January and 14 January at the Waialae Country Club.  With news of Tiger Woods...
  • TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI HOTELI YA WHITE SANDS MAANDALIZI YA AFCON
    TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI HOTELI YA WHITE SANDS MAANDALIZI YA AFCON
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kambini Juni 1 katika hoteli ya White Sands mjini ...
  • MOHAMED SALAH ANAVYOFURAHIA MAISHA LIVERPOOL
    Kiungo Mohamed Salah akifurahia kwenye mazoezi ya Liverpool leo Uwanja wa  Melwood kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England ...
  • UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    Neil Morrice walks you through the front runners for Saturday's feature races at Cambridgeshire, Newmarket and the Cheveley Park Stake...
  • YANGA SC 6-1 KENGOLD (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)
    YANGA SC 6-1 KENGOLD (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)
      from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/Rr0NtG3
  • BETPAWA YAPIGA ‘AMSHA AMSHA’ MWANZA KUELEKEA FAINALI LİGİ YA MABINGWA ULAYA
    BETPAWA YAPIGA ‘AMSHA AMSHA’ MWANZA KUELEKEA FAINALI LİGİ YA MABINGWA ULAYA
    KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya betPawa imezawadia vifaa vya michezo timu mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwa sehemu ya kuchangia maend...
  • YANGA SC 4-0 KAGERA SUGAR (LIGI KUU YA NBZ TZ BARA)
    YANGA SC 4-0 KAGERA SUGAR (LIGI KUU YA NBZ TZ BARA)
      from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2dy3pqT
Copyright Viral Sports: SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA FUNDISHO