Na Mwandishi Wetu, MONACO
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji imepangwa kundi moja na E Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na mabingwa watetezi, Liverpool ya England, Napoli ya Italia na Salzburg ya Austria.
Katika droo ya michuano hiyo iliyofanyika sambamba na tuzo za Mwanasoka Bora Ulaya, Samatta amejikuta akinagushiwa kwenye kundi la mabingwa watetezi, Liverpool na maana yake atakutana tena na Sadio Mane wa Senegal.
Mane aliiongoza Senegal kuichapa Tanzania ya Samatta kwenye mechi ya Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni mwaka huu nchini Misri. Huko walikuwa na Mohamed Salah wa Liverpool, ambaye timu yake, Misri kama Tanzania ilitloewa mapema.
Mbwana Samatta amepangwa kundi moja na Liverpool, Napoli na Salzburg Ligi ya Mabingwa Ulaya
Kundi A linaundwa na PSG ya Ufaransa, Real Madrid ya Hispania, Club Brugge ya Ubelgiji na Galatasaray ya Uturuki, Kundi kuna Bayern Munich ya Ujerumani, Tottenham Hotspur ya England, Olympiacos ya Ugiriki na Red Star Belgrade ya Serbia.
Kundi C linaundwa na Manchester City ya England, Shakhtar Donetsk ya Ukraine, GNK Dinamo ya Croatia na Atalanta ya Italia, Kundi D linaundwa na Juventus ya Italia, Atletico Madrid ya Hispania, Bayer Leverkusen ya Ujerumani na Lokomotiv Moskow ya Urusi.
Kundi E ndio Liverpool, Napoli, Salzburg na KRC Genk, Kundi F kuna Barcelona ya Hispania, Borussia Dortmund ya Ujerumani, Inter Milan ya Italia na Slavia Praha Jamhuri ya Czech, Kundi G lina Zenit ya Urusi, Benfica ya Ureno, Lyon ya Ufaransa na RB Leipzig ya Ujerumani na Kundi H linazikutanisha Chelsea ya England, Ajax ya Uholanzi, Valencia ya Hispania na Lille ya Ufaransa.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Samatta kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuisaidia Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji msimu uliopita.
Lakini msimu uliopita alicheza michuano ya Europa League na timu yake, Genk ilitolewa hatua ya 32 Bora Slavia Prague ya Czech kwa kuchapwa 4-1 nyumbani baada ya sare ya 0-0 ugenini.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2NFA3Gk
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms