Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
TAASISI ya Mfuko wa Emerson's Zanzibar Foundation (EZF) inatarajiwa kutangaza matokeo ya uhakiki wa filamu 21 zilizowaswilishwa kwenye tunzo ya filamu iliyokusudiwa kuendeleza na kukuza Vipaji vya Vijana wa Kizanzibari wanaotengeneza filamu.
Akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, Mwenyekiti wa Mfuko wa Wakfu wa Emerson's Zanzibar Foundation, Said el-Gheithy alisema Wadhamini wa Bodi ya mfuko huo EZF ulipokea jumla ya filamu 21 kutoka Unguja na Pemba zilizoletwa katika tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka. Kati ya hizo filamu Nane (8) pekee ndio zilizokidhi vigezo na sifa zilizowekwa.
"Mwaka huu tunatoa tunzo ya tano....Filamu 21zilizoandaliwa na Vijana wa Kizanzibari kutoka Unguja na Pemba, nane pekee ziliweza kupenya kwenye mchujo, na kuhakikiwa na Jopo la Majaji katika hatua ya mwisho. Matokeo yatatangazwa Julai 4 mwaka huu hapa Unguja." Alisema Mwenyekiti wa EZF, Said el-Gheithy.
Aliongeza kuwa: "Bodi ya Wadhamini ya Emerson Zanzibar Foundation imekuwa na utaratibu wa kutoa tunzo hiyo mwezi wa Julai kila mwaka linapofanyika Tamasha la Filamu za Kimataifa na za Nchi za Majahazi (ZIFF). Lakini mwaka huu Tunzo hiyo itafanyika kupitia mitandao ya kijamii.
"Tunzo ya Tano kwa mwaka huu itafanyika mitandaoni kutokana na janga la Kirusi cha Covid-19.", alimalizia Said el-Gheithy.
Kwa upande wake Meneja Mwandalizi wa shughuli za Tunzo hiyo, Salma Adim alieleza kuwa tayari majaji wamekamilisha kuzikhakiki filamu hizo. Sasa inasubiriwa kutangazwa matokeo.
"Filamu zilizotengenezwa na Chipukizi ndio kauli mbiu ya mwaka huu. Hivyo basi katika filamu hizo 21 ni nane pekee zilizokidhi vigezo....... .", alisema Salma Adim.
Salma Adim aliwataja Majaji Sita ambao ni wabobezi waliohakiki filamu hizo. Nao ni Helen Peeks, Bi. Maryam Hamdan, Lisenka Beetsra na Salum Stika ambao walihakiki hapa Zanzibar. Majaji wengine, Vanessa Victor na Amil Shivji wao walihakiki filamu hizo kwa njia ya mtandao (online).
Alizitaja filamu hizo zilizoingia Nane Bora ni: 'Mashaka', 'Kipaji', 'Urithi wa Mila', 'Youth Africa Life', 'Kijiji changu', 'Fikra yakinifu', 'Hofu ya Subira' na 'Tubadilike'.
Wadhamini wa bodi hiyo wameeleza kuwa, Mpewa mstahiki atatunukiwa fedha, Milioni Mbili (Ml.2), Tunzo maalum ya EZF na cheti cha ushiriki katika tukio adhimu Mjini Unguja.
Tunzo hiyo imekuwa ikitolewa kila mwaka kuibua vipaji vya Vijana wengi Visiwani Zanzibar.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/31BHqWv
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms