Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BINGWA wa mabara wa ngumi za kulipwa uzito wa Super Welter, Hassan Mwakinyo atautetea mkanda wake wa Chama cha WBF Novemba 13 dhidi ya bondia wa Argentina Jose Carlos Paz.
Pambano hayo yamepewa jina la Dar Fight Night yameandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.
Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito huo huo wa Chama cha IBA. Pambano hilo limepangwa kufanyika kwenye ukumbj wa Next Door Arena.
Mkurugenzi wa The Jackson Group Sports Kelvin Twissa amesema siku hiyo mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz, akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya.

Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twisa (wa pili kulia) akiutambulisha mkanda wa mabara wa WBF ambao bondia Hassan Mwakinyo (wa pili kulia) atautetea dhidi ya bondia Jose Carlos Paz Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki. Wa kwanza kulia ni bonda Dulla Mbabe na wa kwanza kushoto ni bondia Zulfa Macho
Twisa alisema kuwa Zarika atazichapa na Patience Mastara wa Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.
Pia siku hiyo, bondia Abdallah Pazi maarufu kwa jina la Dullah Mbabe atacheza na Alex Kabangu wa DR Congo.
Alisema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika mapambano yake.
"Siku hiyo kutakuwa na pambano makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita, Argentina, DR Congo, Kenya, Uganda, Zimbabwe na wenyeji Tanzania watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za kulipwa wataona kitu tofauti kabisa katika mchezo huo, " alisema Twisa.
Alisema kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV na Asas ina uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi kufanya jambo la kihistoria hapa nchini.
"Tunataka kuona mabondia wanaendelea kwa kupata mapambano mengi ya ngumi na kinacho endana na kazi yao, tulifanya kazi na Mwakinyo kwa miaka mitatu na kuona ufanisi wake, tumeamua kuendelea naye na mabondia wengine wa Tanzania, tutaubadili mchezo wa ngumi nchini," alisema.
Kwa upande wake, Mwakinyo alisema kuwa hiyo ni fursa kwake na kuahidi kufanya vyema siku hiyo.
"Namshukuru Twisa na kampuni ya Jackson Group Sports ambao wameonyesha nia ya kuubadili mchezo wa ngumi za kulipwa, sitawaangusha watanzania," alisema Mwakinyo.
Mwakilishi wa WBF nchini Tanzania, Chatta Michael alisema kuwa rais wa shirikisho hilo, Goldberg Howard atasimamia mapambano hayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twisa (katikati) akizungumza wakati wa utambulisho wa mapambano ya Dar Fight Night yaliyopangwa kufanyika Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door Arena kati ya bondia Hassan Mwakinyo (wa pili kulia) dhidi ya bondia Jose Carlos Paz wa Argentina. Wa kwanza kulia ni bonda Dulla Mbabe na wa kwanza kushoto ni bondia Zulfa Macho na pili kushoto ni mwakilishi wa WBF Tanzania, Chatta Michael.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/31aHo74
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang MWAKINYO KUWANIA UBINGWA WA MABARA DHIDI YA MUARGENTINA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2020/10/mwakinyo-kuwania-ubingwa-wa-mabara.html. Terimakasih atas perhatiannya.