• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2026 (127)
    • ►  Maret (18)
    • ►  Februari (42)
    • ►  Januari (67)
  • ►  2025 (318)
    • ►  Desember (70)
    • ►  November (4)
    • ►  September (1)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ▼  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ▼  November (405)
      • Dupavillon blitz puts Dolphins in control
      • AZAM FC YATANGULIA KIPINDI CHA KWANZA, BIASHARA UN...
      • NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN KUSINI 1-0, KUMEN...
      • Impressive Live Instant Wins
      • International Racing: Tuesday 01 December 2020 – N...
      • Neil Morrice: International Racing - Tuesday 1 Dec...
      • Fairview Best Bets & Tips - Tuesday 01 December 2020
      • DIOP WA SENEGAL ALIYEWATUNGUA WAFARANSA 2002 AFARI...
      • Australia vs India: Third ODI Preview
      • South Africa vs England: Third T20I Preview
      • CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA TOTTENHAM STAMFOR...
      • ARSENAL WAPIGWA MECHI YA TANO MSIMU HUU, WACHAPWA ...
      • MSHAMBULIAJI TEGEMEO WA AZAM FC, PRINCE DUBE MPUME...
      • Hollywoodbets Greyville Best Bets - Monday 30 Nove...
      • #HollywoodCyberMonday Twitter Promotion
      • SIMBA SC YAWAZIMA WANIGERIA KWAO, YAWACHAPA PLATEA...
      • CAVANI ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA MABAO MAWILI MAN...
      • Hollywoodbets offers First Person Live Games by Ev...
      • Neil Morrice: UK Best Bets - Monday 30 November 2020
      • MESSI AMUENZI MARADONA BAADA YA KUFUNGA BAO LA NNE...
      • POLISI TZ YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA COASTAL UNIO...
      • International Racing: Monday, 30 November- Australia
      • Betgames Africa Wins of the Week - 29 November 2020
      • MLANDEGE YACHAPWA 5-0 NA CS SFAXIEN YA TUNISIA PAL...
      • HAZARD AUMIA, REAL MADRID YACHAPWA 2-1 NYUMBANI NA...
      • MIKE TYSON AREJEA ULINGONI NA KUMSHUGHULIKIA ROY J...
      • YANGA SC 1-0 JKT TANZANIA (LIGI KUU TANZANIA BARA)
      • NAMUNGO FC WAANZA VYEMA MICHUANO YA AFRIKA, YAWATA...
      • MAHREZ APIGA HAT TRICK MAN CITY YAICHAPA BURNLEY 5...
      • SHA TIN Best Bets - Sunday 29 November
      • International Racing: Sunday 29 November 2020 - Ge...
      • VAR YAKATAA MABAO YA SALAH, MANE LIVERPOOL YATOA S...
      • Neil Morrice: UK Racing Best Bets - Sunday 29 Nove...
      • KASEKE TENA, YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA...
      • SIMBA SC WAKIJIFUA MJINI JOS KABLA YA KUWAVAA PLAT...
      • KIKOSI CHA AZAM FC KILIVYOWASILI MUSOMA LEO TAYARI...
      • CAF YARUHUSU MASHABIKI ASILIMIA 50 KUINGIA MECHI Z...
      • South Africa vs England: Second T20I Preview
      • Australia vs India: Second ODI Preview
      • New Zealand vs West Indies: Second T20I Preview
      • WSB Gauteng Summer Cup 2020 - Full Results All Races
      • IBRAHIM CLASS AMSHINDA KWA POINTI MZAMBIA NA KUTET...
      • AL AHLY YAIPIGA ZAMALEK 2-1 NA KUTWAA TAJI LA TISA...
      • KIKAO CHA MCHAKATO WA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDE...
      • SIMBA SC WALIVYOWASILI JOS LEO TAYARI KUWAVAA WENY...
      • Crazy Time Big Win
      • International Racing: Friday 28 November 2020
      • Neil Morrice: UK Racing Best Bets - Saturday 28 No...
      • Winning Form Best Bets: Kranji - 28 November 2020
      • Hollywoodbets Scottsville Best Bets - Sunday 29 No...
      • Turffontein Best Bets - Saturday 28 November 2020
      • Kenilworth Best Bets - Saturday 28 November 2020
      • Black Friday: 20% Deposit Bonus
      • MAELFU WAMZIKA DIEGO MARADONA MAKABAURI YA BELLA V...
      • ARSENAL YAICHAPA MOLDE FK 3-0 NA KUTINGA 32 BORA E...
      • AZAM FC YAWATUPIA VIRAGO MAKOCHA WAKE WAROMANIA BA...
      • BALOZI WA TANZANIA NCHINI NIGERIA AWATEMBELEA SIMB...
      • NGORONGORO HEROES YAITANDIKA SOMALIA 8-1 NA KUTING...
      • International Racing: Friday 27 November 2020
      • French Top 14: Round 10 Preview
      • PRO14: Round 8 Preview
      • Gallagher Premiership: Round 2 Preview
      • F1 2020: Bahrain Grand Prix Preview
      • Hollywoodbets Greyville Best Bets - Friday 27 Nove...
      • Fairview Best Bets & Tips - Friday 27 November 2020
      • PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU B...
      • Neil Morrice: International Racing - Friday 27 Nov...
      • 2020 WSB Gauteng Summer Cup: Final Field Betting
      • English Premier League: Gameweek 10 Preview
      • Autumn Nations Cup: Round 3 Preview
      • Currie Cup: Round 1 Preview
      • Vaal Best Bets - Thursday 26 November 2020
      • SIMBA SC WAWASILI SALAMA ABUJA TAYARI KUWAVAA PLAT...
      • ATALANTA WAICHAKAZA LIVERPOOL MABAO 2-0 PALE PALE ...
      • BAYERN MUNICH WAENDA 16 BORA BAADA YA KUICHAPA RB ...
      • MANCHESTER CITY WAICHAPA OLYMPIAKOS 1-0 PIRAEUS LI...
      • REAL YAICHAPA INTER MILAN 2-0 NA KUITUPA NJE LIGI ...
      • Neil Morrice: International Racing - Thursday 26 N...
      • Chelsea vs Tottenham Preview
      • NYOTA WA SIMBA SC WALIVYOONDOKA ADDIS ABABA LEO AS...
      • CAF Champions League Final: Zamalek vs Al Ahly Pre...
      • PWD Bamenda vs Kaizer Chiefs Preview
      • DStv Premiership: Gameweek 5 Preview
      • New Zealand vs West Indies: First T20I Preview
      • Australia vs India: First ODI Preview
      • South Africa vs England: First T20I Preview
      • Spanish La Liga: Gameweek 11 Preview
      • European/Sunshine Tour - Alfred Dunhill Championsh...
      • German Bundesliga: Gameweek 9 Preview
      • Italian Serie A: Gameweek 9 Preview
      • Dolphins hampered by bad light at Kingsmead
      • Black Friday Wishlist Promotion: Ts and Cs
      • HAALAND APIGA MBILI BORUSSIA DORTMUND YAIPIGA CLUB...
      • NEYMAR AFUNGA BAO PEKEE PPSG YAWACHAPA1-0 RB LEIPZIG
      • RONALDO AFUNGA JUVENTUS YATOKA NYUMA NA KUSHINDA 2...
      • BRAITHWAITE AFUNGA MAWILI BARCELONA YASHINDA 4-0 U...
      • GIROUD AFUNGA LA USHINDI CHELSEA YAWALAZA RENNES 1...
      • BRUNO FERNANDES APIGA MBILI MANCHESTER UNITED WASH...
      • COASTAL UNION YAZINDUKA NA KUICHAPA IHEFU SC 1-0 M...
      • TFF YAKANA KUPOKEA MGAWO WA RAIS WA CAF ALIYEFUNGI...
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ►  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE » BURIANI KAPTENI MALIKI FAKI, MTU MUHIMU KATIKA HISTORIA YA YANGA

BURIANI KAPTENI MALIKI FAKI, MTU MUHIMU KATIKA HISTORIA YA YANGA

Na Dk Ramadhani Kitwana Dau, DAR ES SALAAM
JUMATANO ya tarehe 11 Novemba 2020 ni siku ambayo soka la Tanzania limepatwa na pigo kubwa kwa kuondokewa na mmoja wa watu waliohifadhi kumbukumbu nyingi sana kuhusu soka la Afrika Mashariki.
Ilikuwa saa 4 na dakika 2 usiku kwa saa za Malaysia (saa 11 na dakika 2 jioni kwa saa za Tanzania) wakati mwanangu Ahmad Ramadhani Dau aliponitumia ujumbe mfupi uliosema “Assalaam Alaykum. Captain Malik amefariki”. Mara tu nilipopata ujumbe huo nikajua kuwa umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia ya kumuenzi Captain Maliki pamoja ya kuwa kuandika Taazia si jambo ambapo nalifurahia kwa sababu ambazo nimeshazieleza huko nyuma. Lakini Waswahili wanasema “lisilobudi hutendwa”. Kwa kuwa hii si mara yangu ya kwanza kuandika Taazia, mrejesho (feedback) ambao nimekuwa nikipata kutoka kwa wasomaji mbalimbali na hata baadhi ya Wahariri ni kuwa Taazia zangu ni ndefu sana. Kwa sababu hiyo, Taazia hii itakuwa fupi ingawa kwa kufanya hivyo ninajua kuwa nitawakosesha wasomaji mambo mengi ambayo marehemu Capt. Maliki aliwahi kunisimulia wakati wa uhai wake. 


Captain Maliki alizaliwa tarehe 15 Oktoba 1936 kisiwa cha Kwale Wilaya ya Mkuranga (karibu na Kisiju). Alikuwa ni kati ya watoto wawili (yeye na dada yake Mgeni binti Faki Abdallah) wa Mzee Faki Abdallah na mkewe Bi Mwanaviwa binti Mwinyimadi Mkendwa. Ndugu zake wengine alizaliwa nao mama mmoja ambao ni: Mzee bin AbdulRahman bin Maalim, Yahya bin AbdulRahman bin Maalim, Mwanahamisi binti AbdulRahman bin Maalim, Amina binti AbdulRahman bin Maalim na Mwatumu binti AbdulRahman bin Maalim. Captain Maliki alikuja Dar es Salaam mwaka 1955 na alifikia Mwembetogwa (kwa jina la sasa hivi “Fire”), kwenye nyumba ya marehemu Thabit Iddi maarufu John Iddi (baba yake Iddi John). Kikazi, katika umri wake wote, Capt. Maliki aliajiriwa na Public Works Department (PWD) kama fundi wa vitasa vya milango. Mimi nilibahatika kumfahamu Capt. Maliki tokea nikiwa mtoto mdogo wa chini ya umri wa miaka 6 kwa sababu nilizaliwa, nilelewa na niliishi Mwembetogwa.  Wakati huo Capt. alikuwa akijulikana kwa jina la utani Dr. Nnamdi Azikiwe (maarufu “Zik”) ambaye alikuwa Rais wa Nigeria kati ya mwaka 1963-1966.
Jina kamili la marehemu Capt. Maliki ni Maliki Faki Abdallah lakini kwa muda wote wa uhai wake alijulikana zaidi kama Capt. Maliki ingawa kwa watu wachache sana wakimjua pia kwa jina la Dr. Nnamdi Azikiwe. Marehemu Capt. Maliki alianza kujishughulisha na mpira akiwa mchezaji wa African Boys ambayo ilikuwa timu B ya Yanga (Young Africans).   Alikuwa namba 4 na nahodha wa timu na ndio sababu ya kupata jina la Captain. Akiwa mchezaji wa African Boys na baadae Yanga, Capt. Maliki alitoa mchango mkubwa sana haswa kwenye klabu ya Yanga kwa kuwaleta wachezaji ambao baadae walikuwa maarufu sana na wengine walichezea timu ya Taifa kwa miaka kadhaa. Baadhi ya wachezaji ambao Captain Maliki aliwashawishi na kuwafuata yeye mwenyewe kuwaleta Dar es Salaam kuchezea timu ya Yanga ni marehemu Athumani Kilambo (a.k.a Baba watoto, ambaye alimfuata Bagamoyo) marehemu Maulidi Bakari Dilunga (ambaye alijulikana kwa majina ya utani matatu, “Eusebio”, “Mexico” na “DDT” yaani Dilunga Dangerous Ten, alimfuata Mzumbe Sekondari alipokuwa anasoma), Abuu Marwa (baadae alikwenda kucheza Cosmopolitan), marehemu AbdulRahman Juma (a.k.a mapafu ya mbwa, kwa muda mrefu sana alikuwa Captain wa Yanga, Dar es Salaam combine na timu ya Taifa) Brian Segatwa, Semboko nk. Wengi kati ya wachezaji hao ndio waliokuwa msingi wa timu iliyoifunga Sunderland 5-0 mwaka 1968. 
Mwenyezi Mungu Alimjaalia Capt. Maliki kipaji cha ajabu cha kutunza kumbukumbu ghibu. Alikuwa ana uwezo wa kupanga timu za Taifa za Kenya, Tanganyika, Uganda na Zanzibar za mashindano ya Gossage (baadae Challenge Cup) kwa miaka ya 1950, 1960 na 1970.   Hali ilikuwa ni hivyo hivyo kwenye timu za vilabu vya Cosmo, Simba, TPC, Yanga, nk. Uwezo wake haukuishia kwenye kupanga listi ya timu hizo, bali alikuwa na uwezo wa kusimulia jinsi mechi zilivyochezwa, timu gani ilivaa jezi ya aina gani, timu ziliingia uwanjani saa ngapi, timu ipi ilitangulia kuingia uwanjani, matokeo yalikuwa vipi, nani waliofunga magoli na katika dakika ya ngapi. Msemaji wa Simba Haji Sunday  Manara hakukosea aliposema mara kadhaa kuwa Capt. Maliki alikuwa  Encyclopedia ya mpira wa Afrika Mashariki. 
Yapo mengi sana ambayo Dr. Nnamdi Azikiwe alinisimulia ambayo yanasisimua sana. Lakini kwa uhaba wa nafasi, leo nitasimulia kisa kimoja tu. Kwenye kisa hiki, Capt. Maliki alikuwa anajaribu kunionesha ni namna gani wapenzi wa mpira wa zamani walivyokuwa na mapenzi makubwa na timu zao tofauti na ilivyo hivi sasa. Captain anasimulia kuwa mwaka 1955/1956 kulikuwa na mechi baina ya Sunderland (sasa Simba) na Yanga. Wakati huo Sunderland ilikuwa ina mchezaji kiungo mshambuliaji hodari sana akiitwa Kilima Abdallah Huni ambaye pia alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanganyika.  Siku chache kabla ya mechi, Kilima akapatwa na kesi ambayo  baadhi ya watu waliitakidi kuwa alibambikiwa na wapenzi wa Yanga ili awekwe rumande au afungwe jela na akose kucheza mechi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa. Ikumbukwe kuwa miaka hiyo mechi ya Sunderland na Yanga ilikuwa inachezwa mara moja tu kwa mwaka. Kwa hiyo timu ikifungwa inabidi isubiri mwaka mzima kabla haijapata nafasi ya kulipiza kisasi. 
Kesi ikapelekwa kwa Hakimu anaitwa Nassoro Kiruka, Mzee wa Kimanyema na mwanachama mkubwa wa Yanga na alikuwa akiogopwa sana. Mwanawe alikuwa anaitwa Selemani Kiruka mwanachama mwanzilishi wa Pan Africa Football Club. Wakati kesi inaendelea kusikilizwa ghafla aliinuka Bwana Yahaya Kiambwe (mwenyeji  wa Rufiji) ambaye alikuwa mshabiki mkubwa wa Sunderland na kumwambia Hakimu kuwa anaomba kesi ya Kilima apewe yeye na ikibidi afungwe yeye ili Kilima aachiwe huru kwa sababu kesho yake Sunderland inacheza na Yanga na Kilima ni mchezaji ambaye wanamtegemea sana kwenye mechi hiyo! Captain Maliki anasema mapenzi ya vilabu yalifikia hatua hiyo. Hatimaye Kilima aliachiwa huru na akacheza mechi dhidi ya Yanga. Capt. Maliki anasimulia kuwa mchezo ulikuwa mkali sana na wenye ushindani mkubwa haswa kwa vile washabiki wa Simba waliamini kuwa kulikuwa na njama za kumfanya Kilima akose mechi ile. Mpira ulipokwisha kuna timu ilishinda 1-0. Wakati naandika Taazia hii, kwa kupitia simu ya Mohamed Rishad (Adolf), nilizungumza na Bwana Yusuf Salum Maleta aliyekuwa beki wa kulia wa Sunderland akiwa nyumbani kwake Kinondoni, Mkwajuni.  Yeye alikithibitisha kisa hiki na kunitajia jina la mchezaji aliyefunga goli. Je ni timu ipi iliyoshinda? Nani alifunga goli? Fumbo hili nakuachia wewe msomaji. 
Jambo ambalo limenisikitisha sana ni kuondoka Capt. Maliki bila kuacha urithi wake kwa kizazi cha sasa na vijavyo. Wakati wa uhai wake mimi na Mohamed Saidi tulimuomba sana aandike kumbukumbu hizo na Mohamed alijitolea kuifanya kazi hiyo kwa njia ya mahojiano na baadae aiweke vizuri katika mfumo wa kitabu. Kwa wale wote waliopata bahati ya kumjua na kuzungumza na Capt. Maliki kuhusu masuala ya mpira Afrika Mashariki wataelewa umuhimu wa kuweka kumbukumbu hizo kwa sababu baadhi ya mambo aliyokuwa anayazungumza huwezi kuyapata kwenye vitabu au nyaraka zozote.  Kwa mfano wapi unaweza kupata rekodi ya timu ipi ilitangulia kuingia uwanjani na kwa sababu gani, timu ipi iliingilia mlango gani na kwa sababu ipi, mchezaji yupi alitangulia kushuka kwenye gari, mchezaji yupi alitangulia kuingia uwanjani na alitanguliza mguu upi. Wapi leo utapata kumbukumbu inayoeleza kwa nini mechi ya Sunderland na Yanga iliyochezwa kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa (sasa uwanja wa Uhuru)  mwaka 1969, timu zote tatu (ndiyo ni timu tatu) zilifika uwanjani mapema lakini mchezo ulichelewa kuanza hadi saa 12 jioni? Kwa nini Maulidi Bakari Dilunga (Eusebio) alitoka nje mara tu baada ya kufunga goli dakika 15 za kipindi cha kwanza? Na kwa nini Dilunga aliambiwa na viongozi wa Yanga aondoke kabisa uwanjani aende nyumbani kwake Magomeni mtaa wa Ubungo wakati mechi inaendelea? Kwa mpira wa zamani hayo yote yalikuwa na sababu na umuhimu wake katika kutafuta ushindi lakini si rahisi kuyapata kwenye vitabu vya historia. Marehemu Capt. Maliki alikuwa anasimulia kisa hiki na visa vingine vingi utadhani vimetokea jana. Capt. Maliki pia ana kumbukumbu ya mwaka ambao klabu ya SIMBA ilikuwa na Makamu Mwenyekiti Juma NYATI na kocha kutoka Hungary John FARU. Pia alikuwa anakumbuka alichokisema mchezaji wa Brazil Pele kuhusu Maulidi Dilunga kuwaambia marehemu Johnson Mbwambo (Katibu Mipango wa Yanga) na marehemu Ibrahim Pazi (Mweka Hazina wa Yanga) walipokwenda Brazil kusaini Mkataba wa kuileta timu ya Santos (akiwemo na Pele) kuja Tanzania kama wageni wa Yanga. Bahati mbaya Captain Maliki hakuwahi kuzikusanya kumbukumbu zake kwa njia ya kitabu mpaka umauti ulipomfika na kurejea kwa Mola Wake. Ushauri kama huo nimempa Mohamed Rishad “Adolf” kwa sababu baada ya Capt. Maliki mtu mwingine mwenye kumbumbuku nzuri sana ni yeye. Lakini kwa jinsi ninavyomfahamu rafiki yangu huyu wa miaka 48 (tokea 1972) nina hakika hatofanya hivyo. 
Jambo lingine la kusikitisha kufuatia msiba huu ni kukosekana kwa viongozi wa Yanga kwenye maziko ya Capt. Maliki. Nimesema ni jambo la kusikitisha (sio kwamba nawalaumu) kwa sababu kwa bahati mbaya viongozi wa Yanga na hata vilabu vingine vikongwe hawajui historia yao.  Nina hakika wanachama na hata viongozi wa Yanga wa sasa hawamjui Capt. Maliki alikuwa nani na alitoa mchango gani kwenye klabu yao. Hili limedhihiri kwangu kiasi miaka 4 au 5 iliyopita wakati niliposoma kwenye Gazeti la Yanga Imara ambalo nadhani ni Gazeti rasmi la klabu ya Yanga. Katika toleo hilo mwandishi amezungumzia mgogoro wa Yanga uliopelekea kuanzishwa kwa timu ya Pan Africa. Mwandishi amedai kuwa mgogoro huo ulianza mwaka 1973 wakati Yanga walipofungwa goli 1-0 kwa goli lilofungwa na Haidari (Muchacho) kufuatia kross ya Wellington Mwaijibe. Baada ya mechi hiyo ikazuka tafrani na hatimaye kuanzishwa timu ya Pan Africa. Hili sio kweli kabisa. Inashangaza sana kuona klabu kubwa kama Yanga inashindwa kuwa na historia sahihi ya maisha yake. Kama mgogoro wa Yanga ulianza 1973, je wakati wa mechi ya Simba na Yanga ya Nyamagana Mwanza Agosti 1974 timu ya Pan Africa ilikuwa wapi na nani walikuwa wanachezea timu hiyo?  Je wakati wa mechi ya Simba na Yanga Januari 1975 Zanzibar, timu ya Pan ilikuwa wapi? Na je Yanga ilipokwenda kutetea kikombe cha Afrika Mashariki Januari 1976 Mombasa, timu ya Pan ilikuwa wapi na nani walikuwa wachezaji wake? Majibu ya maswali yote hayo ni kwa timu ya Pan Africa ilikuwa haijaanzishwa! Mgogoro wa Yanga ulianza baada ya mechi ya Yanga na Enugu Rangers ya Nigeria mwezi Mei 1975. Habari yake ni ndefu na hapa si mahala pake. 
Natoa wito kwa vilabu vikubwa viandike historia ya timu zao tokea zilipoanzishwa na zijenge utamaduni wa kuwaenzi watu waliotoa mchango mkubwa katika kuanzishwa na kuendelezwa kwa timu hizo. Bado muda upo kwa sababu baadhi ya wazee wenye kumbukumbu bado wapo hai na Mwenyezi Mungu Awape umri mrefu zaidi ili tuvune uzoefu na busara zao. Baadhi ya wazee hao ni mjomba wangu Jabiri Katundu (Yanga) mjomba wangu Akherina Katundu (Simba), Yusuf Salum Maleta (full back wa Sunderland), Mustafa Choteka (namba 10 Sunderland), Hamisi Kilomoni (half back Sunderland) Emmanuel Albert Mbele (Yanga baadae Simba center forward) Gilbert Mahinya (Sunderland baadae Yanga half back) n.k. Aidha natoa wito kama huo kwa TFF (ambapo mimi ni mmoja wa Wadhamini) waandike historia ya timu ya Taifa tokea wakati wa ukoloni hadi hivi sasa. 
Buriani Capt. Maliki Fakih Abdallah a.k.a Dr. Nnamdi Azikiwe. Mwenyezi Mungu Ailaze roho yake mahala pema.   
Innallillah Wainnaillahi Rajiuun.  Sisi sote ni Waja wa Mwenyezi Mungu, na Kwake Yeye ndio marejeo yetu.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Hn2sjX best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang BURIANI KAPTENI MALIKI FAKI, MTU MUHIMU KATIKA HISTORIA YA YANGA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2020/11/buriani-kapteni-maliki-faki-mtu-muhimu.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 05.11
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17
    SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17
    Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM  KOCHA Mkuu wa timu ya wanawake u-17  ya Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa kikosi kimejipanga kufanya v...
  • MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MTANZANIA Alice Gyunda miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha taj...
  • TUZO ZA LIGI KUU ZABORESHWA, SASA WACHEZAJI KUPEWA NA KING'AMUZI CHA AZAM TV
    Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura, akionyesha tuzo atakayokuwa akipewa Mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vod...
  • BARCELONA 3-1 ALAVES
    BARCELONA 3-1 ALAVES
    from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2s2Iqyx
  • CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    BAO pekee la beki wa kimataifa wa England, Ben Chilwell dakika ya 45 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford Uwanja wa...
  • ARSENAL YAMUONGEZEA MSHAHARA SANCHEZ ASIENDE BAYERN MUNICH
    KLABU ya Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates. Ofa mp...
  • EPL: Week 36 Preview
    EPL: Week 36 Preview
    We preview week 36 of the 2017/18 English Premier League season which is set to get underway on Saturday 28 April.  We’re into the final s...
  • YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    KLABU ya Yanga imewasimamisha wachezaji wake wawili, Dickson Ambundo na Mrundi Saido Ntibanzokiza kuelekea mechi ya Fainali ya Kombe la S...
  • ENGLAND YALAZIMISHWA SARE WEMBLEY
    ENGLAND YALAZIMISHWA SARE WEMBLEY
    WENYEJI, England wamelazimishwa sare ya 1-1 na Hungary katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwan...
  • Hollywoodbets Extends Horse Racing Sponsorship with Grooms' Initiative
    Hollywoodbets Extends Horse Racing Sponsorship with Grooms' Initiative
    Hollywoodbets have extended their original R10 million three-year sponsorship of Gold Circle by a further R1.5 million per year with the an...
Copyright Viral Sports: BURIANI KAPTENI MALIKI FAKI, MTU MUHIMU KATIKA HISTORIA YA YANGA