Na Anitha Jonas – WHUSM, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amewataka viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo kuwa wabunifu na kuandaa mikakati ya kukuza na kuendeleza michezo nchini.
Dkt. Abbas ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Warsha ya Wadau wa Michezo nchini ya kutoa maoni ya katika rasimu ya Kanuni za Taifa za Kupinga mbinu haramu na matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni (Anti Doping).
Akizungumza katika Warsha hiyo Katibu Mkuu huyo na Msemaji Mkuu wa Serikali alisisitiza kuwa kila kiongozi wa Chama na Mashirikisho ya Michezo atimize wajibu wake kwa kutoa maoni ili kujiepusha na kero ya wanamichezo kuja kufungiwa kushiriki michezo na kuliletea taifa aibu.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Yusuph Singo akiwasihi Wadau wa Michezo kulichukulia kwa uzito suala la Anti Doping na kuharakisha utoaji maoni, ili kuepusha taifa kufungiwa ushiriki wa michezo ya Kimataifa, Novemba 19, 2020, Jijini Dar es Salaam, katika ufunguzi wa Warsha ya kutoa maoni ya rasimu ya kanuni zitakazo asiliwa za kupinga mbinu haramu za matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini, waliyohudhuria Warsha ya kutoa maoni ya Rasimu ya Kanuni zitakazoasiliwa za kupinga mbinu haramu za matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni iliyofanyika leo Novemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam.
“Najua mnafahamu kuwa taasisi hii ya kupinga matumizi ya mbinu haramu na dawa za kuongeza nguvu michezoni namna ilivyo na nguvu hivyo ni vyema suala hili mkalifanya kwa umakini, ili kuiepusha nchi kuwekewa vikwazo vya kushiriki michezo mbalimbali kimataifa,” alisema Dkt.Abbasi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Michezo Tanzania Bw.Yusuph Singo alisema Kamati ya Anti Doping kwa sasa imefanya kazi ya kuandaa kanuni ambazo zitakazo asiliwa na kuwa za kitaifa na badae serikali itaunda sheria ya kusimamia masuala hayo ya kupinga mbinu haramu michezoni.
“Kenya walisitishiwa kushiriki mashindano ya Kimataifa kwa kukosa “codes” ambazo zinaendana na mazingira ya nchi yao, ambazo ndiyo hizi kanuni tulizoandaa hivyo, ningependa suala hili tulichulie uzito na tulikamilishe haraka ili kuepusha taifa na chagamoto kama hii na tungependa kanuni hizi zianze kutumika mapema mwakani,” alisema Bw.Singo.
Halikadhalika nae Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Philbert Bayi aliishukuru Serikali kwa kufanikisha kusainiwa kwa mkataba huo wa kupinga matumizi ya mbinu haramu michezoni mnamo mwaka 2017, kwani Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi chache zilizokuwa bado hazijasaini mkataba huo.
Pamoja na hayo Dkt. Abbasi aliwaeleza viongozi wa Vyama vya Michezo kuwa mwanzoni mwa mwezi Desemba amepanga kutembelea vyama mbalimbali vya michezo nchini, kwa lengo la kufahamu changamoto na mikakati ya kukuza michezo ambapo alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano inataka kuacha alama katika michezo hivyo watoe hoja za nini kifanyike ili kuendeleza michezo mbalimbali kwa nchini.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/331YnJD
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms