KOCHA wa Tunisia, Mondher Kebaier ametaja kikosi cha wachezaji 26 kuelekea mchezo na Tanzania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2021.
Kiungo wa Zamalek, Ferjani Sassi na beki wa kushoto wa Al Ahly, Ali Maaloul watakaokutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwezi huu ni miongoni mwa waliojumuishwa kikosini.
Kebaier pia amewaita Youssef Msakni, Wahbi Khazri na Nabil Makni katika safu yake ya ushambuliaji.
Beki wa AEK Athens, Nassim Hnid alirejeshwa kikosini kabla ya kupimwa na kukuta na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, hivyo kuenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Saddam Ben Aziza wa Etoile du Sahel.
Beki wa Le Havre, Ayman Ben Mohamed ambaye ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili na Esperance yumo kikosini pia.
Tai wa Carthage watamenyana na Taifa Stars Ijumaa wiki hii Uwanja wa Hamadi Agrebi Olimpiki mjini Rades, kabla ya kurudiana nao Dar es Salaam siku nne baadaye.
Tunisia inaongoza Kundi J kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Tanzania na Libya zenye pointi tatu kila moja, wakati Equatorial Guinea ambayo haina pointi inashika mkia.
Kikodi kamili cha Tunisia ni, makipa: Farouk Ben Mustapha (Esperance), Moez Ben Chrifia (Esperance), Ayman Dahmen (CS Sfaxien) na Elyes Damerji (Stade Rennais, Ufaransa)
Mabeki: Wajdi Kechrida (Etoile du Sahel), Mohamed Dräger (Olympiakos, Ugiriki) Yassine Meriah (Rizespor, Uturuki), Dylan Bronn (Metz, Ufaransa), Saddam Ben Aziza (Etoile du Sahel), Montassar Talbi (Rizespor, Uturuki), Oussema Haddadi (Kasımpaşa, Uturuki) na Ali Maaloul (Al Ahly, Misri)
Viungo: Ferjani Sassi (Zamalek, Misri), Ellyes Skhiri (FC Cologne, Ujerumani), Anis Ben Slimane (Brondbiy IF, Denmark), Aymen Ben Mohamed (Le Havre, Ufaransa), Seifeddine Khaoui (Olympique de Marseille, Ufaransa), Naim Sliti (Al-Ittifaq, Saudi Arabia), Marc Lamti (Hannover, Ujerumani), Elyes Jlassi (US Monastir), Hamza Rafia (Juventus, Italia), Mohamed Amine Ben Amor (Etoile du Sahel), Saad Bguir (Abha, Saudi Arabia)
Washambuliaji: Wahbi Khazri (Saint-Étienne, Ufaransa), Nabil Makni (Chievo Verona, Italia), Youssef Msakni (Al-Duhail, Qatar)
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2JWp1wO
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms