MWANASOKA Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borrusia Dortmund ya Ujerumani, atatetea tuzo yake dhidi ya Waalgeria wawili, Riyad Mahrez na Islam Slimani wote wa Leicester City ya England.
Hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutoa orodha ya wachezaji watano wa mwisho wa kuwania tuzo hiyo.
Wengine wawili wanaowania tuzo hiyo ni Sadio Mane wa Senegal na Liverpool na Mohamed Salah wa Misri na Roma baada ya kupigiwa kura na Wajumbe wa Kamati ya Habari ya CAF, Kamati ya Ufundi na Maendeleo na nusu ya Wajumbe 20 maalum (Wajumbe 10).
Katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, ambayo inashikiliwa na Mtanzania Mbwana Samatta wachezaji wanne wa Mamelodi Sundowns wameingia fainali.
Hao ni Khama Billiat wa Zimbabwe, Keegan Dolly, Hlompho Kekana wa Afrika Kusini na Denis Onyango wa Uganda ambao watachuana na mchezaji mmoja wa TP Mazembe, Rainford Kalaba wa Zambia.
Katika hatua ya mwisho kura zitapigwa na Makocha wakuu wa timu za taifa za nchi 54 wanachama wa CAF, zikiwemo wanachama washifiki kama visiwa vya Reunion na Zanzibar pamoja na Wajumbe 10 maalum.
Usiku wa tuzo za CAF 2016 utafanyika Januari 5, mwaka 2017 mjini Abuja, Nigeria chini ya udhamini wa kampini ya simu ya Globacom.
Samatta hajaingia kutetea tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika kwa sababu alihamia KRC Genk ya Ubelgiji mapema mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2fBifII
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms