Na Princess Asia, MTWARA
SIMBA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC jioni ya Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Ushindi huo, unaifanya Simba ifikishe pointi 38 baada ya kucheza mechi 16, ikiwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Josephat Bulali na Mohamed Mkono, dakika 45 za kwanza zilimalizika bila mabao.
Kiungo mpya wa Simba James Kotei kutoka Ghana alilazimika kumpisha Muzamil Yassin dakika ya 19 baada ya kuumia kufuatia kugongana na Nahodha wa Ndanda, Kiggi Makasi.
Muzamil Yassin ameseti bao moja na kufunga moja Simba ikishinda 2-0 Mtwara leo
Kipa Mghana wa Simba alifanya kazi ya ziada dakika ya 20 kumzuia mshambuliaji chipukizi wa Ndanda, Riffat Khamis asifunge baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki.
Dakika saba kabla ya mapumziko, mshambuliaji wa Simba Ibrahim Hajib alipiga shuti zuri la mpira wa adhabu ambalo liliupita ukuta wa Ndanda, lakini likatoka nje sentimita chache.
Kipindi cha pili, Ndanda ilipata pigo dakika ya 52 baada ya beki wake Hemd Khoja kuumia na kushindwa kuendela na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Benito John.
Pengo la Khoja lilionekana wazi kuiathiri Ndanda, kwani baada ya hapo Simba wakaanza kuipenya ngome ya wenyeji wao kwa urahisi na kupata mabao mawili.
Mshambuliaji Muivory Coast wa Simba, Frederick Blagnon hakuamini macho yake dakika 59 baada ya mpira wa kichwa alioupiga kuunganisha krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuokolewa vizuri na kipa Jeremiah Kasubi.
Dakika moja baadaye, winga Shizza Kichuya akamdakisha kipa Kasubi shuti dhaifu la karibu ndani ya sita kufuatia pasi ya Mo Ibrahim.
Hatimaye Muzamil Yassin akaifungia Simba bao la kwanza kwa shuti kali dakika ya 63 akimalizia pasi ya Mo Ibrahim.
Baada ya bao hilo, Ndanda walionekana kupoteana na kuwaruhusu Simba kuuteka zaidi mchezo.
Hata hivyo. kuanzia dakika ya 80, Ndanda walitulia kidogo, ingawa Simba waliendelea kutawala mchezo.
Mo Ibrahim akaifungia Simba bao la pili dakika ya 91 akimalizia pasi ya kiufundi ya Muzamil.
Kikosi cha Ndanda FC kilikuwa; Jeremiah Kisubi, Kiggi Makassy, Bakari Mtama, Paul Ngalema, Hemed Khoja/Benito John dk53, Salvatory Ntebe, Nassor Kapama, Salum Minelly, Salum Telela, Omar Mponda/Helbert Lukindo dk77 na Riffat Khamisi.
Simba; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei/Muzamil Yassin dk19, Frederic Blagnon/Laudit Mavugo dk62, Ibrahim Hajib/Said Ndemla dk51 na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na kuishusha Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. Lakini Simba inaweza kurejea kileleni kesho ikishinda dhidi ya wenyeji, Ndanda FC mjini Mtwara.
Shujaa wa Yanga leo alikuwa ni winga Simon Happygod Msuva aliyefunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya kuseti moja kipindi cha kwanza.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Heri Sasii aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lililokuja baada ya muda mrefu wa timu zote kushambuliana kwa zamu, lilifungwa na beki Michael Aidan Pius aliyejifunga dakika ya 38 katika harakati za kuokoa krosi ya Simon Msuva iliyokuwa inafuatiliwa vizuri na winga Deus Kaseke.
JKT Ruvu pamoja na kuondoka uwanjani baada ya nusu ya kwanza wakiwa nyuma, lakini walicheza vizuri na kupeleka mashambulizi mawili ya hatari langoni mwa Yanga ambayo yaliokolewa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.
Yanga nayo ilicheza vizuri pia, lakini wachezaji wake walishindwa kutengeneza nafasi nzuri za kufunga katika kipindi cha kwanza zaidi ya hiyo waliyotumia kupata bao la kwanza.
Dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili, kocha Mzambia wa Yanga, George Lwandamina alimtoa mshambuliaji Amissi Tambwe na kumuingiza kiungo Said Juma ‘Makapu’.
Mabadiliko hayo yaliifanya Yanga ianze kutawala sehemu ya kiungo na kupika mashambulizi yenye shibe hatimaye kupata mabao mawili zaidi.
Msuva alifunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 57 akimalizia krosi ya Kaseke baada ya kazi nzuri ya kiungo mwenzake Haruna Niyonzima. Msuva tena akafunga bao la tatu dakika ya 90 akimalizia pasi ya Niyonzima dakika ya 90.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm alikuwepo jukwaa kuu kufuatilia mchezo, wakati kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu alikuwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini.
Baada ya mchezo, kocha Lwandamina alisema timu haijaanza kucheza kwa kiwango chake kwa kuwa bao anajaribu wachezaji.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Mzima. Mwadui imeilaza 1-0 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City imelazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Ruvu Shooting imetoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Geoffrey Mwashiuya dk84, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Said Juma ‘Makapu’ dk55na Deus Kaseke.
JKT Ruvu: Hamisi Seif, Michael Aidan, Edward Charles, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon/Naftal Nasho dk66, Rahim Juma, Ally Bilal/Mussa Juma dk77, Hassan Dilunga, Najim Magulu, Atupele Green/Saad Kipanga dk77 na Edward Joseph.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2hxfTyt
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms