Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor 'Cheche' amesema kwamba anajua namna ya kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri kwenye Fainali ya Kombe la Mapinduzi kesho Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC jioni ya jana ya kujiandaa na mchezo huo, baada ya Azam kuingia fainali kwa kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo Frank Domayo Jumanne.
“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche.
Kikosi cha Azam kilichoifunga Yanga 4-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi B
Alisema katika mazoezi ya kwanza wachezaji wa kikosi hicho wameyaanza vema wakiwa na furaha na mwanzo mpya huku akidai kuwa licha ya ushindani utakaoonyeshwa kwenye mchezo huo wamejipanga kukabiliana na hali hiyo.
Cheche ambaye atakiongoza kikosi hicho kama kocha mkuu hadi kumalizika kwa michuano hiyo kabla ya kumpisha Kocha Mkuu mpya wa Azam FC aliyetambulishwa jana, Aristica Cioaba raia wa Romania, mpaka sasa amekiongoza kikosi hicho kuandika rekodi ya aina yake ya kutofungwa mchezo wowote wala kuruhusu bao.
Hadi inaingia fainali kwa kuitoa Taifa ya Jang’ombe, Azam FC kwenye hatua ya makundi iliichapa Zimamoto bao 1-0, ikatoa suluhu na Jamhuri kabla ya kuifumua Yanga mabao 4-0, ukiwa ni ushindi wa kihistoria tokea timu hizo zianze kukutana.
Azam FC kesho Alhamisi jioni itamalizia mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuivaa Simba kwenye mchezo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya Watanzania wapenzi wa soka.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2jlyMmx
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang KOCHA AZAM ASEMA; "KUMFUNGA SIMBA KAMA KUMSUKUMA MLEVI". Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/01/kocha-azam-asema-kumfunga-simba-kama.html. Terimakasih atas perhatiannya.