Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka ya FIFA kwa miaka minne ijayo. Uteuzi huo unaanza mwaka huu 2017 hadi 2021.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Januari 18, 2017 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura inasema: “Tuna faraja kukufahamisha kuwa umeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya FIFA. Tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa uteuzi huu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino (kulia)
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Kamati hiyo inayoongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Bara la Asia, ina majukumu ya kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.
Wajumbe wengine wote watatangazwa kwenye tovuti ya FIFA ambayo ni www.FIFA.com.
Huu ni mfululizo wa Tanzania kupata nafasi katika vyombo vikubwa vinavyoendesha soka FIFA na CAF. Mwishoni mwa mwaka jana, CAF – Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika lilimteua Rais Malinzi kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu inayoongozwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou ya kuboresha mfumo wa uongozi wa CAF.
TFF inamshukuru Rais Gianni Infantino na kamati yake ya ushauri kwa kumteua Malinzi katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo muhimu ya maendeleo ya soka ulimwenguni.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2k7LsB2
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms