Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA imewafuata watani, Simba SC kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi sita na mabao nane ya kufunga ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa na kuendelea kuongoza Kundi B.
Yanga ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa mabao hayo mawili, yote yakifungwa na winga wake machachari wa kulia, Simon Happygod Msuva aliyeibuka mchezaji bora wa mechi.
Msuva alifunga bao la kwanza dakika ya 11 akimalizia mpira wa adhabu wa Nahodha na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima kumtungua kipa Mwinyi Abbas.
Bao la pili na la nne kwake katika mashindano hayo alifunga dakika ya 21 akiiwahi pasi ndefu ya Thabani Kamusoko na kumtoka beki Shaffi Rajab kabla ya kumchambua tena Mwinyi Abbas.
Kipindi cha pili, Yanga ilirudi vizuri tena na kuendelea kutawala mchezo, lakini hawakuwa na bahati ya kupata mabao zaidi.
Msuva aliyefunga mabao mawili pia katika mchezo wa kwanza Yanga ikiichapa Jamhuri 6-0, alishindwa kukamilisha hat trick katika mchezo wa leo baada ya kukosa penalti kipindi cha pili.
Penalti hiyo ilitolewa na refa Waziri Shekha baada ya Msuva mwenyewe kuangushwa na beki Hassan Hajji Ali kwenye boksi.
Msuva alipiga mkwaju wa penalti ukapanguliwa na kipa Mwinyi Hamisi na kumkuta tena winga huyo wa Yanga, ambaye alipoupiga tena ukagonga mwamba kabla ya kuondoshwa kwenye hatari.
Mchezo mwingine wa Kundi A kati ya Jamhuri na Azam utafuatia Saa 2:30 usiku, wakati kesho michuano hiyo itaendelea kwa mechi za Kundi A KVZ na Jang'ombe Boys Saa 10:00 jioni na Simba dhidi ya mabingwa watetezi, URA Saa 2:30 usiku.
Yanga itarudi dimbani Jumamosi kumenyana na wapinzani wao wakuu wa mataji nchini, Azam kuanzia Saa 2:30 usiku kukamilisha mechi za Kundi A.
Kikosi cha Yang leo kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima na Emanuel Martin.
Zimamoto; Mwinyi Hamisi, Yussuf Mtuba, Hassan Ali, Suleiman Juma, Shaffi Rajab/Suleiman Abbad dk32, Hajji Nahodha, Hassan Saidi, Makame Mbwana, Hakim Ali/Ally Salum dk18, Ibrahim Ahmada na Hamad Vuai.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2hSLUAz
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang YANGA YAIFUATA SIMBA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/01/yanga-yaifuata-simba-nusu-fainali-kombe.html. Terimakasih atas perhatiannya.