Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES ZALAAM
VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga leo wamegawana pointi baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Simba na Yanga zote zinafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi nane kila moja – maana yake Ligi Kuu msimu imekuwa ya ushindani zaidi, vigogo hao wakichuana na Azam FC na Mtibwa Sugar kileleni.
Yanga ndiyo waliolazimika kupigana kusawazisha bao kupitia kwa mshambuliaji wake, Mzambia, Obrey Chirwa baada ya winga Shiza Kichuya kuanza kuwafungia Simba, mabao yote yakipatikana kipindi cha pili.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Heri Sasii ambaye mara kadhaa alikuwa akilalamikiwa na wachezaji wa Yanga uwanjani kwa uchezeshaji wake, Kichuya alifunga bao lake dakika ya 57 kwa kichwa baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa wana Jangwani, kabla ya kuonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda kwa kwenda kushangilia mbali.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani dakika tatu baadaye Yanga walisawazisha kupitia kwa Chirwa aliyefunga kwa kichwa baada ya pasi ya winga Geoffrey Mwashiuya.
Sasii pia aliwaonyesha kadi za njano wachezaji wa Yanga beki Juma Abdul dakika ya 70 na mshambuliaji, Ibrahim Ajib dakika ya 69 wote kwa kupingana na maamuzi yake.
Pamoja na sare hiyo, Yanga ndiyo waliotengeneza nafasi zaidi dhidi ya wapinzani wao, lakini umaliziaji wao mbaya uliwanyima japo bao la kuongoza.
Lakini ni Simba ndiyo walioanza kulitia misukosuko lango la Yanga dakika ya 22, baada ya mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi kuunganishia nje krosi nzuri ya beki wa kulia, Erasto Nyoni.
Yanga wakajibu dakika ya 23 baada ya kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi kufumua shuti kali lililokwenda nje sentimita chache baada ya kuukuta mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula wa Simba kufuatia shuti la Mwashiuya.
Tshitshimbi tena dakika ya 30 akafumua shuti kali baada ya kuukuta mpira uliookolewa na mabeki wa Simba kufuatia shuti la mpira wa adhabu la beki Juma Abdul.
Dakika ya 31 Chirwa aliondoka vizuri na mpira kutokea katikati ya Uwanja hadi nje kidogo ya boksi na kufumua shuti lililokwenda juu ya lango la Simba hadi upande wa pili.
Kipindi cha pili, timu zote zilionekana kuja na mbinu mpya katika kusaka mabao, safari hii Yanga ndiyo walioanza kuwashitua Simba baada ya Mwashiuya kufumua shuti kali dakika ya 55 ambalo liliokolewa na Manula.
Baada ya mabao mfululizo Kichuya akianza dakika ya 57 na Chirwa akifuatia dakika ya 60, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, ingawa tahadhari iliongezeka.
Beki Mganda, Juuko Murshid alijitwisha vizuri kona ya kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima kujaribu kuifungia Simba bao la pili dakika ya 66, lakini mpira ukaenda juu ya lango la Yanga.
Yanga wakajibu dakika ya 68 baada ya Ajib kufumua shuti kali kufuatia pasi ya Tshtishimbi, lakini mpira ukaenda nje.
Winga Emmanuel Martin aliyetokea benchi kipindi cha pili aliikosesha Yanga bao la ushindi dakika ya 71 baada ya kupiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa Manula kufuatia krosi ya Chirwa.
Yanga wakapandishia shambulizi lingine mwishoni mwa dakika hiyo, lakini Ajib tena akapiga shuti ambalo liliokolewa ns mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyetokea benchi.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshitshimbi, Pius Buswita, Raphael Daudi/Pato Ngonyani dk65, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Geoffrey Mwashiuya.
Simba SC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, James Kotei/Jonas Mkude dk75, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk84, Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo/John Bocco dk75 na Haruna Niyonzima.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2yZjQEK
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang YANGA YAIVIMBIA SIMBA, SARE 1-1 MABAO YA KICHUYA NA CHIRWA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/10/yanga-yaivimbia-simba-sare-1-1-mabao-ya.html. Terimakasih atas perhatiannya.