KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ametajwa kwenye ripoti ya Polisi kwamba anachunguzwa juu ya harakati za kupigania Uhuru wa Katalunya kujitenga kutoka Hispania.
Wanaharakati Jordi Sanchez na Jordi Cuixart waliwekwa rumande Oktoba mwaka huu kwa kuongoza harakati hizo, jambo ambalo ni kuvunja sheria za Hispania.
Wamekuwa wakichunguzwa kwa mienendo yao na watu wanaoshirikiana nao na taarifa zinasema Guardiola anahusika na anaweza kupandishwa Mahakama Kuu mbele ya Jaji Pablo Llaren.
Guardiola anafahamika wazi kama anaunga mkono kampeni za Katalunya kuwa nchi inayojitegemea kwa kujitenga kutoka Serikali ya Hispania yenye makao yake makuu Madrid.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akiuhutubia umati wa maelfu ya watu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kocha huyo wa City alihudhuria mbio maalum za harakati hizo, 'Pro-independence Rally' mjini Barcelona hivi karibuni pamoja na Carles Puigdemont, Rais wa Serikali ya Katalunya na watu wengine 10,000.
Aliuambia umati kwamba atapiga kura ya Uhuru Oktoba 1 'hata kama nchi ya Hispania haitataka hilo'.
Hata hivyo, kura hizo hazikutambuliwa na Madrid, Polisi wa Hispania wameanza uchunguzi juu ya mtu huyo maarufu ambaye alithubutu kutoa maoni yake mbele ya umma.
Taarifa ya Polisi, iliyonukuliwa kwenye gazeti la Kispaniola la El Nacional, ilisema kwamba 'kampeni ziliongozwa na Josep Guardiola na alithubutu kuwaambia wafuasi wote wapiganie Uhuru'.
Zoezi hilo lilifanyika Oktoba 1 na wasiasa wa Pro-Independence, Oriol Junqueras na Joaquim Forn na wanaharakati Jordi Sanchez na Jordi Cuixart mara moja waliswekwa rumande.
Rais wa Katalunya, Carles Puigdemont alikimbilia mji wa Brussels nchini Ubelgiji na ameambiwa atakamatwa pia akirejea Hispania.
Guardiola amekuwa akivaa lebo ya njano kama sehemu ya kampeni zake za kutaka wanasiasa na wanaharakati waliokamatwa waachiwe na hivi karibuni alisema: "Kama UEFA ama FIFA, au Ligi Kuu (England) wanataka kuniadhibu mimi kwa kuvaa lebo ya njano wafanye hivyo. Ninanvaa hii kwa ajili ya watu wawili ambao wapo jela kwa sababu ya kutetea haki ya kupiga kura,".
Malalamiko ya kuvaa lebo ya kuunga mkono harakati za Katalunya kujitenga yaliibuliwana kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hivi karibuni.
Mourinho alihoji kwa nini mpinzani wake huyo wa muda mrefu anaruhusiwa kuvaa lebo hiyo na akashauri mambo ya kisiasa yasiingizwe kwenye michezo.
UEFA imekwishabadili sheria zake msimu huu na sasa ujumbe wa ishara tu ndiyo unaruhusiwa – ambayo inatumika pia na FA - na kwa maana hiyo Guardiola alikuwa huru kuvaa lebo hiyo.
Katalunya walitarajiwa kupiga kura jana kuchagua uongozi mpya wa Serikali yao, zoezi ambalo linatarajiwa kuleta mgawanyiko zaidi.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2DtViDN
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms