• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2025 (243)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ▼  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ▼  Oktober (535)
      • MAN CITY LEO WANA KAZI NA FULHAM ETIHAD CARABAO CUP
      • Dolphins Fight Back on Day Three in Cape Town
      • BARCELONA YASHINDA 1-0 UGENINI KOMBE LA MFALME
      • KOCHA WA MUDA AREJESHA FURAHA REAL MADRID, YASHIND...
      • SON HEUNG-MIN AFUNGA MAWILI KUIPELEKA SPURS ROBO F...
      • GUENDOUZI ALIMWA KADI NYEKUNDU ARSENAL YASHINDA 2-...
      • CHELSEA YATUPA NJE TIMU YA LAMRAD KOMBE LA LIGI EN...
      • SAMATTA AFUNGA MABAO MAWILI KRC GENK YATOKA NYUMA ...
      • KOCHA PAWASA ATAJA KIKOSI CHA FAINALI ZA AFRIKA SO...
      • KMC YAISHINDILIA NDANDA FC 3-0 NA KUJIINUA KIDOGO ...
      • R1 Million Horseracing Cash Promotion: Terms and C...
      • Vaal Thursday 1 November 2018 Best Bets
      • ATP Tour 2018: Paris Masters Preview
      • Telkom Knockout: Quarterfinal Preview
      • English Premier League: Week 11 Preview
      • US PGA Tour: Shriner’s Hospital for Children Open ...
      • The European Tour: Turkish Airlines Open Preview
      • International Rugby: Ireland v Italy Preview
      • Opinion: Mindfulness and Cricket, a Perfect Marriage
      • Italian Serie A: Week 11 Preview
      • NFD: Week 10 Preview
      • MOHAMMED ISSA ‘BANKA’ KUANZA KUICHEZEA YANGA FEBRU...
      • German Bundesliga: Week 10 Preview
      • Pro14: South African Matches Preview Round 8
      • BAYERN MUNICH WAIPIGA 2-1 TIMU YA DARAJA LA NNE KO...
      • New Zealand 2019 Super Rugby Squads Confirmed
      • Mourinho Taunter Fined by FA
      • Real Madrid Players are Hurting
      • YANGA SC 1-0 LIPULI FC (LIGI KUU TZ BARA)
      • Greyville Wednesday 31 October 2018 Best Bets
      • Fired up Abbott Excited to be Back in Durban
      • Dolphins Made to Work Hard on Day Two at Newlands
      • Dyantyi Nominated for Breakthrough Player of the Y...
      • YANGA SC YAREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA ...
      • MBAO FC CHUPUCHUPU KUPIGWA TENA KIRUMBA, YACHOMOA ...
      • India v West Indies: Fifth ODI Preview
      • International Rugby: England v South Africa Preview
      • R10m Pot up for Grabs in the Mzansi Super League
      • Julen Lopetegui Sacked by Real Madrid
      • TFF KUSAFIRISHA WAANDISHI WA HABARI 15 KWA BASI KW...
      • Chetty & Frylinck put Dolphins in sound position
      • Breeders' Cup Classic 2018 - Final Field
      • MAHREZ AFUNGA BAO PEKE MAN CITY YAWAPIGA 1-0 TOTTE...
      • KOCHA WA TIMU B ARITHISHWA MIKOBA YA LOPETEGUI ALI...
      • MWADUI FC WAWATWANGA WAPINZANI WAO WA SHINYANGA NA...
      • Kenilworth Best Bets - Tuesday 30 October 2018
      • 5 Talking Points from the Sporting Weekend
      • Lucky Numbers Draw Times & Results
      • Pakistan v New Zealand: First T20I Preview
      • ATP Tour: Masters 1000 Series Selected Ro64 Matches
      • To 13 Reactions - Currie Cup Final 2918
      • MSEMAJI WA SIMBA SC, HAJJI SUNDAY MANARA ATEULIWA ...
      • HIDAYA JUMA AWA MWANAMKE WA PILI KUJISHINDIA BAJAJ...
      • SA Horse Racing Preview - 29th Oct to 1st Nov 2018
      • No Messi, No Problem - Top 22 El Clasico Reactions
      • WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE HELIKOPTA YA MMILIKI ...
      • Lewis Hamilton Fifth Title Win - Reactions
      • Leicester City Confirm Passing of Chairman
      • Few Changes for Dolphins Ahead of Newlands Outing
      • Flamingo Park Monday 29 October 2018 Best Bets
      • SAMATTA AFUNGA BAO BADO KIDOGO GENK ISHINDE, IKASA...
      • MBAPPE ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA PSG WAIPIGA 2-0 MA...
      • MAHOJIANO YA BIN ZUBEIRY NA QUREISH UFUNGUO
      • MAHOJIANO YA BIN ZUBEIRY NA HEMED MATOBANGO
      • RUVU SHOOTING 0-5 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)
      • SINGIDA UNITED 0-1 AZAM FC (LIGI KUU TZ BARA)
      • MAHOJIANO YA BIN ZUBEIRY NA MWANAMTWA KIHWELO
      • SUAREZ APIGA HAT TRICK BARCELONA YAIFUMUA REAL MAD...
      • CHELSEA YAENDELEZA UBABE, YAICHAPA 4-0 BURNLEY PAL...
      • PENALTI MBILI ZAIKOSESHA USHINDI ARSENAL, YATOA SA...
      • POGBA AFUNGA LA KWANZA, ASETI LA PILI MAN UNITED Y...
      • MMILIKI WA LEICESTER CITY AFARIKI DUNIA NDANI YA H...
      • OKWI AFUNGA HAT TRICK SIMBA SC YAISHUGHULIKIA KIKA...
      • BBC YARIPOTI MMILIKI WA LEICESTER ALIKUWEPO KWENYE...
      • NGOMA AFUNGA BAO PEKEE NAMFUA AZAM YAICHAPA 1-0 SI...
      • MGOMBEA UENYEKITI WA BODI AAHIDI MAMBO MAZURI SIMB...
      • WANARIADHA WA TANZANIA BARA WATAMBA MBIO ZA KILOMI...
      • TANZANIA YAPANGWA KUNDI MOJA NA SENEGAL, NIGERIA N...
      • PROMOTA MSANGI ADAI MFAUME MFAUME ALIONEWA NA REFA...
      • TUMPOKEE NINJE NA KUMPA USHIRIKIANO KWA MANUFAA YA...
      • MATOBANGO AKIWA NA MACHUPPA NA AKILIMALI BAADA YA ...
      • Pakistan v Australia 3rd T20I Preview
      • India v West Indies: Fourth ODI Preview
      • HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER CITY YATEKETEA M...
      • RONALDO AFUNGA MABAO MAWILI JUVE YATOKA NYUMA NA K...
      • SANCHO AFUNGA TENA MABAO MAWILI DORTMUND YATOA SAR...
      • MANE AFUNGA MAWILI, SALAH NA SHAQIRI MOJA MOJA LIV...
      • MLINDA MLANGO PETER MANYIKA ‘JUNIOR’ ASAINI MKATAB...
      • Durban Heat Ready to Heat up 031
      • Greyville Sunday 28 October 2018 Best Bets
      • 1voucher at PEP Facebook Promotion – Win a R200 1v...
      • Fairview Sunday 28 October 2018 Best Bets
      • Turffontein Saturday 27 October 2018 Best Bets
      • Kenilworth Best Bets - Saturday 27 October 2018
      • ‘PANGA PANGUA’ RATIBA LIGI KUU YAENDELEA, SAFARI H...
      • 2018 ATP Tour: ATP 500 Series Selected Quarter Fin...
      • 2018 ATP Tour: ATP 500 Series Selected Quarter Fin...
      • India v West Indies: Third ODI Preview
      • Sri Lanka v England: Only T20I Preview
      • Jwayelani Promotion: Win 1 of 2 R500 Shopping Vouc...
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE » MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA TAIFA

MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA TAIFA

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
ULE msemo wa “Sisi Na Wao Lini”  umetimia jana baada ya miamba miwili ya Jiji la Dar es Salaam, Simba na Yanga kushuka kwenye Uwanja wa Taifa na kutunishiana misuli ndani ya dakika 90, kila mmoja akimuonyesha mwenzake nani zaidi.
Watani hao wa Dar es Salaam waliona isiwe kesi, wakaamua kumaliza mchezo kama walivyoanza kwa kutoka suluhu.
Mchezo wa Simba na Yanga maarufu kama Watani wa Jadi wa Dar es Salaam, ama Kariakoo Derby (Makao Makuu wa Simba yapo Kariakoo na Yanga ilianzishwa Kariakoo kabla ya kuhamia Jangwani) kwa kawaida tumezoea kukutana na vituko na mambo mengi ya kushangaza katika mchezo huu, hii ni kutokana na uhasimu mkubwa ulio katika klabu hizi.
Ukitaka kufurahia mchezo huu, wahi kufika uwanjani usisubiri wakati wa mtanange kuanza, mimi nilijitahidi kuwahi mapema kabla ya mchezo nikawa Uwanja wa Taifa kushuhudia mambo ya nje ya uwanja kabla ya mchezo wenyewe uwanjani.
Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akimpita beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' katika mchezo wa jana

Katika pitapita zangu nikamuona bwana mmoja anayefahamika kwa jina la Frank Yanga ameshika mdoli wenye muonekano wa mnyama Simba kwa kutumia kinywa chake, nikatabasamu kabla sijaondoa macho yangu katika kinywa cha kijana yule aliyekua amejitanda kitambaa kikubwa chenye rangi ya njano na kijani ghafla nikaona kipara kilichoandikwa kwa rangi ya
kijani 2-0.
Nikaona hapana jambo hili haliwezi nipita bure nikamfuata kijana yule, nikamuuliza haya yote maana yake nini? Akanijibu hapa mnyama (Simba) keshakufa ndiyo maana nimemning’iniza mdomoni.
Akaniambia Ibrahim Ajib na Amissi Tambwe ndiyo watakaofanya hayo mauaji, basi mimi nikajua tafsiri ya ule mchoro wa kichwani na mdoli uliokua unaning’inia mdomoni.
Basi nikaendelea na pepesa pepesa zangu nikapishana na mtu aliepigilia mavazi mekundu mithili ya mtu alijeruhiwa na chui. Sasa ikabidi niwe makini katika kumpekua japo kwa kutumia macho yangu naweza kugundua ni vitu vingapi alivyovaa venye rangi ile.
Nikaanzia miguuni alikuwa kavaa viatu vyekundu, soksi ndefu hadi magotini nyekundu, suruali nyekundu iliyochomekewa ndani ya zile soksi, fulana kuuuubwa nyekundu iliyochomekewa ndani ya suruali na kofia nyekundu na nyeupe iliyofanana na kawa ya kufunikia chakula ikiwa imefunika kichwa kidogo mithili ya tunda la ubuyu, bwana yule kaona kama haitoshi kaamua kujifunika na shuka kama bendera. 
Nikasema
Mungu msaidie kijana wako apate ushindi asije kurudi kwake akiwa mtupu. Zikiwa zimesalia dakika chache sana mtanange kuanza kama ilivyo desturi wageni waalikwa walisogea katika uwanja kusalimia na kutambulishwa kikosi cha Simba na Yanga kilichokuwa kimesimama
kusubiri filimbi ya Muamuzi.
Viongozi wote waliosalimia akiwemo Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Vituko ni sehemu ya maisha, basi mwamuzi Jonesia Rukyaa akapuliza kipyenga kuashiria mtanange kuanza. Ibrahim Ajib yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga mpira huo ambapo alipiga pasi ndefu kuelekea upande wa Simba mpira uliotoka nje moja kwa moja bila kuguswa na mchezaji
yeyote.
Mpira ukawa wa kurusha kuelekezwa upande wa Yanga na aliyerusha mpira ule alikuwa Shomari Kapombe, ndani ya dakika saba uwanja ukainamia upande wa Yanga kana kwamba mkandarasi wa uwanja angeweza kutafutwa aulizwe hilo bonde hakuliona wakati wa ujenzi wa uwanja au alifanya
kusudi?
Dakika ya 11 Mganda Emmanuel Okwi alifanya shambulizi hatari sana lakini ashukuriwe mlinda mlango wa Yanga, Beno Kakolanya aliyesimama imara, Okwi akaona haitoshi dakika ya 18 akafanya shambulizi jingine Beno akaokoa.
Simba walionekana kusaka alama tatu, dakika ya 26 walishapata kona tatu huku Yanga ikiwa haina ilichopata, nakumbuka shuti moja alilopiga Ajib dakika ya 22 akiwa umbali wa mita 25 kuelekea golini mwa Simba lakini mpira ukapita juu ya lango la Simba.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika milango yote ikiwa imenuna, zikaanza tena dakika 45 za kipindi cha pili mambo yakawa kama yale ya dakika za kwanza kilichobadilika ni wachezaji na upande wa timu kufungia kubadilika.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera dakika ya 55 alimtoa Ibrahim Ajib akamuingiza Matheo Anthony,  Mbelgiji wa Simba Kocha Patrick Aussems akamjibu Zahera dakika ya 62 akamuingiza Mohamed Ibrahim akamtoa Shiza Kichuya lakini bado mambo yakawa yaleyale.
Dakika ya 78 Yanga ikamtoka Deus Kaseke akaingia Mrisho Ngassa, Simba wakajibu tena shambulizi hili dakika ya 81 akatoka Clatous Chama akaingia Said Ndemla, Simba wanazidi kukazia dakika ya 89 akatoka Emmanuel Okwi akaingia Adam Salamba, hadi dakika 90 zinakamilika ubao
wa matokeo ukasoma 0-0.
Haikuwa rahisi kuelewa Simba wamemalizaje mchezo ule bila kupata bao na Yanga wamemalizaje mchezo ule bila kufungwa, Simba walionyesha soka safi sana yawezekana hawakuwahi kucheza soka kama lile tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara na Yanga walicheza mchezo wa ajabu sana
yawezekana hakuwahi kucheza mchezo ule tangu kuanza kwa ligi.
Ngoja nikwambie mwanzo mwisho mpira umechezwa na Simba kama ningekuwa kipimo cha umiliki wa mipira ningetoa asilimia 90 kwa Simba na 10 kwa Yanga, kibarua nilichokuwa nimebakiwa nacho ni kuwatafuta makocha wa timu hizi mbili.
Safari yangu ilianzia kwa Kocha wa Simba aliyekuwa na maneno machache tuu ya kujieleza japo alionekana kushangazwa na matokeo waliyoyapata licha ya kutengeneza nafasi nyingi
“Kiukweli sielewi kwa nini hatujashinda tumetengeneza nafasi nyingi sana tumemiliki mpira ndani ya dakika 90 kikubwa tunahitaji kuwa makini ukizingatia wiki mbili zilizopita hatujawa na matokeo mazuri,” anasema Aussems.
Mambo yakawa tofauti kwa Kocha wa Yanga, Zahera aliyekuwa na mengi sana ya kuzungumza tena alizungumza kiufundi.
 “Wanasema kama huwezi kushinda mechi basi usipigwe hicho ndicho kilichonifurahisha tatizo limekuja wachezaji wengi walipotea sababu nilibadilisha mfumo tuliozoea kucheza katika mechi nne tulizocheza awali.
“Tuliangalia video ya Simba mara nne vile tulivyoona ndivyo walivyocheza leo (jana) tuliamua kuwaachia wacheze mpira maana wao wana presha tofauti na sisi, tumeshinda michezo minne tofauti na Simba hivyo tukasema tutawaachia watengeneze nafasi nyingi.
“Wametengeneza nafasi nyingi za kupata magoli kwa sababu sisi dhamira yetu ni kuwaachia wacheze mpira mtu akipoteza mpira unapaswa utoke spidi, ukiangalia Kaseke na Ajib wanalala hilo lilikua tatizo letu ila sare matokeo haya mimi nayafurahia tu,” anasema Zahera.
Yanga walionekana wakicheza mchezo wa kuzuia zaidi tofauti na Simba waliokua wakitafuta mabao, Simba iliimarika kuanzia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji ndiyo sababu ya wao kutengeneza mashambulizi mengi zaidi kuliko Yanga.
Mchezo wa jana umenishangaza sana kama kuna  mchezaji aliyestarehe ndani ya uwanja ni kipa wa Simba, Aishi Manula alistarehe sana alichokifanya ni kukamilisha idadi ya wachezaji 11 kwa kikosi kwani alitulia bila kupata kashikashi nyingi kama kipa wa Yanga.
Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya huyu ndiye mchezaji ambaye hakupata hata muda wa kukumbuka anaitwa nani, muda wote alikuwa akipambana na wachezaji wa Simba waliokuwa wakiagiza mafataki langoni mwake.
Simba imecheza michezo sita ikishinda mara tatu, ikatoka sare mara mbili na kupoteza mara moja na sasa ina pointi 11, Yanga imecheza mechi tano, imeshinda mara nne na kutoka sare moja hivyo sasa ina pointi 13.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2IuZF4e best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA TAIFA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2018/10/mambo-yalivyokuwa-katika-mechi-ya-simba.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 08.30
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Stand a chance to win your share of R100 000 cash! Play R5 or more using your Hollywoodbets account on the selected Lucky Numbers draws an...
  • SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    VIUNGO, Muivory Coast Aubin Kramo Kouamé (kushoto) na José Luis Miquissone wa Msumbiji wakiwa kwenye mazoezi ya Simba leo Uwanja wa Mo Si...
  • Lucky Numbers Draw Times & Results
    Lucky Numbers Draw Times & Results
    All the information you need for the 501 Lotto draws offered by Hollywoodbets for Lucky Numbers and Powa Numbas betting! Get closing times...
  • Bafana held by Nigeria in AFCON Qualifier
    Bafana held by Nigeria in AFCON Qualifier
    Bafana Bafana moved one step closer to the 2019 Africa Cup of Nations with a point in their 1-1 draw with Nigeria at the FNB Stadium on Sa...
  • French Top 14: Toulouse v La Rochelle Preview
    French Top 14: Toulouse v La Rochelle Preview
    Toulouse can qualify for a 27th French domestic final with a semi-final victory over La Rochelle at the Stade Matmut-Atlantique on Saturda...
  • Hollywoodbets REFER A FRIEND Bonus
    Hollywoodbets REFER A FRIEND Bonus
    HOW TO REFER A FRIEND TO HOLLYWOODBETS Get R50 FREE when you Refer A Friend to Hollywoodbets.mobi! Learn how to participate in this promo...
  • Winning Form Promotion - Jockey Trainer Combo
    Winning Form Promotion - Jockey Trainer Combo
    You could win a R200 Hollywoodbets betting voucher. Simply comment on the competition post who is your favourite jockey, trainer combo of ...
  • Kenilworth Best Bets - Saturday 7 April 2018
    Kenilworth Best Bets - Saturday 7 April 2018
    Winning Form brings you their best tips for Kenilworth's racing on Saturday the 7th of April 2018. Tips provided by Winning Form, a...
  • UEFA Champions League: Matchday 3 Preview
    UEFA Champions League: Matchday 3 Preview
    Our football writer previews the UEFA Champions League matchday three action which kicks off on Tuesday 23 October 2018. Matchday three o...
  • Daily Predictor Game: Stand A Chance To Win Your Share of R10 000 In Cash And Betting Vouchers
    Daily Predictor Game: Stand A Chance To Win Your Share of R10 000 In Cash And Betting Vouchers
    Stand a chance to win your share of R10 000 in cash and betting vouchers by playing our new Daily Predictor Game. R200 betting vouchers da...
Copyright Viral Sports: MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA TAIFA