Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
NYOTA aliyeng’ara katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki michuani ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Maurice Michael anatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 8, mwaka huu kwenda Denmark kujiunga na klabu ya FC Midtjylland ya Ligi Kuu ya huko.
Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba hiyo ni sehemu ya mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwapeleka wachezaji Serengeti Boys Ulaya kujiunga na klabu mbalimbali kucheza soka la kulipwa.
Mbali na Michael, wengine saba waliopo kwenye mpango wa kupelekwa Ulaya hivi karibuni ni Kelvin John, Bernard Pastory, Agiri Ngoda, Edson Mshirakandi, Salum Milinge, Pascal Msindo na Alphonce Mabula ambao wote waling’ara kwenye michauno ya CECAFA AFCON Qulifyng Agosti mwaka huu, Tanzania ikiambulia nafasi ya pili baada ya kufungwa na Uganda kwenye fainali.
Na hatua hiyo inakuja wakati Serengeti Boys ikiwa inajiandaa kwa michuano ya AFCON U17 itakayofanyika Mei mwakani mjini Dar es Salaam.
“Michael ndiye atakuwa mchezaji wa kwanza kuondoka huku wachezaji wengine saba wakifuatia baadae, mazungumzo na klabu za barani Ulaya yanaendelea na tumefikia sehemu nzuri. Huu ni mpango maalumu wa kuhakikisha tunakuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje, ambao watakuja kuwa msaada mkubwa hapo baadaye,”amesema Milambo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2xS1bJQ
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms