KLABU ya Manchester United inatarajiwa kumtambulisha mchezaji wake wa zamani, Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wake wa muda.
Jana usiku, kiasi cha saa 12 baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho, tovuti ya United iliposti video yenye maelezo: 'Solskjaer anakuwa kocha wetu wa muda, misimu 20 tangu tuchukue mataji matatu kwa bao hili Camp Nou...’.
Video hiyo ambayo inakumbushia bao la ushindi la mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1999, haikutokea kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti hiyo ya klabu bali ilipostiwa URL yake.
Manchester United inatarajiwa kumtambulisha Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wake wa muda kuchukua nafasi ya Jose Mourinho
Baadaye United waliondoa habari hiyo lakini wanatarajiwa kuipandisha tena mara kocha huyo wa Molde atakapotambulishwa rasmi kumrithi Mourinho kumalizia msimu.
Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg mara moja aliandika ujumbe wa kumpongeza Solskjaer usiku wa jana katika tweet ambayo baadaye aliifuta.
Solskjaer, aliyefunga zaidi ya mabao 100 katika miaka yake 11 ya kuichezea klabu ya Old Trafford, atasaidia na aliyekuwa Msaidizi namba mbili wa Sir Alex Ferguson, Mike Phelan kumalizia msimu.
Lakini inafahamika kwamba kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino anabaki kuwa mtu anayetakiwa kwa muda mrefu na United na vyanzo vimekwishaweka wazi juu ya dhamira yake kufanya kazi Old Trafford.
Muargentina huyo alikuwa chaguo la Sir Ferguson kabla ya Mourinho kuajiriwa mwaka 2016 na inafahamika United imekiwshafanya jaribio la kumng’oa Spurs, lakini watakutana na kikwazo kutoka kwa mkuu wa Tottenham, Daniel Levy, aliyemsainisha mkataba wa miaka mitano mwezi Mei.
Hakuna namna ya kukwepa kumnunua na maana yake Man United watalazimika kulipa Pauni Milioni 40 kumpata mtu wamtakaye.
Watakutana pia upinzani kutoka kwa Real Madrid ambao walikuwa tayari kumpa ofa kocha huyo wa zamani wa Espanyol mwenye umri wa miaka 46 ahamie Bernabeu.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2UU05qK
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms