WENYEJI, Yanga wameweka hai matumaini ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Haikuwa ushindi mwepesi kwa mabingwa hao wa Tanzania, Yanga baada ya TP Mazemba, mabingwa mara tano wa michuano kuanza kupata bao dakika ya 16 likifungwa na kipa Msenegal, Alioune Badara Faty kwa penalti kufuatia beki Mkongo, Chadrack Issaka Boka kumchezea rafu beki wa Kimataifa wa Mauritania, Ibrahima Keita mzaliwa wa Mali.
Ikawa siku nzuri kwa mshambuliaji mzawa, chipukizi wa umri wa miaka 20, Clement Francie Mzize aliyefunga mabao mawili dakika ya 33 na 60, huku bao lingine la Yanga likifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 56.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya tatu, ikiishushia nafasi ya nne TP Mazembe inayobaki na pointi zake mbili baada ya wote kucheza mechi nne.
Al Hilal Omdurman inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na MC Alger yenye pointi nne na wastani mzuri wa mabao zaidi ya Yanga baada ya wote kucheza mechi tatu.
Saa 4:00 usiku wa leo Al Hilal Omdurman watamenyana na MC Alger Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott nchini Mauritania katika mchezo wa nne baina yao wa kundi hilo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/vPJC8iO
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms