NYOTA wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), Hasheem Thabeet amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) katika uchaguzi uliofanyoka leo Jijini Dodoma.
Thabeet ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 34 kati ya 60 zilizopigwa na kwenye Mkutano huo uliosimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Wengine waliochaguliwa ni Mohamed Kisui aliyeshinda nafasi ya Makamu wa Rais, Mwenza Fiston Kabinda (Katibu Mkuu) na Saimon Mirondo (Katibu Msaidizi).
Thabeet ndiye Mtanzania pekee kuwahi kucheza Ligi ya NBA ambako alichezea timu za Memphis Grizzlies kati ya 2009 na 2011, Houston Rockets kati ya 2011 na 2012, Portland Trail Blazers mwaka 2012 na Oklahoma City Thunder kati ya 2012 na 2014.
Thabeet alianza kucheza NBA baada ya kuchaguliwa na Memphis Grizzlies kama chaguo la pili kwa ujumla katika Draft ya NBA mwaka 2009 akiwapiku James Harden na Stephen Curry ambao baadaye wamekuwa wachezaji wakubwa katika historia ya NBA.
Aliingia kwenye Draft hiyo baada ya kufanya vizuri akiwa anachezea timu ya Chuo Kikuu cha Connecticut, Connecticut Huskies katika mashindanio ya Vyuo ambako alikuwa ana wastani kufunga pointi 6.2 na blocks 3.8 kwa mchezo mmoja.
Thabeet hakuanza kucheza mpira wa kikapu utotoni hadi alipofikisha umri wa miaka 15, baada ya kuvutiwa na mchezo huo akiwa mtazamaji na alipojiunga na Sekondari ya Makongo Jijini Dar es Salaam ndipo alianza kucheza timu ya Outsiders.
Alijiendeleza zaidi baada ya kupata nafasi ya kwenda kusoma Shule ya Kikristo ya Cypress huko Houston, Texas alikohitimu mwaka 2006 na kwenda Connecticut.
Pamoja na kuwa Rais wa TBF, kwa sasa Thabeet anachezea Dar City inayocheza Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu Tanzania (NBL) ambayo imefuzu kucheza Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) msimu wa 2026 ambayo itafanyika ukumbi wa BK Arena Jijini Kigali, Rwanda kuanzia Machi 27 hadi Mei 31.
from BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE https://ift.tt/K1NLgD9
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang HASHEEM THABEET RAIS MPYA WA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2026/03/hasheem-thabeet-rais-mpya-wa-mpira-wa.html. Terimakasih atas perhatiannya.