MCHEZAJI mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala ya Ligi Kuu ya England anahofiwa kufa katika ajali ya ndege iliyotokea usiku wa jana katika anga la Uingereza.
Sala aliposti picha sambamba na maelezo 'kwaheri ya mwisho' kwa wachezaji wenzake wa zamani, saa kadhaa kabla ya ndege maalum aliyokodiwa kuanguka maeneo ya England.
Mshambuliaji huyo Muargentina alikamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 15 kujiunga na Cardiff City Jumamosi kabla ya kurejea Ufaransa kuaga katika timu yake ya zamani, Nantes inayoshiriki Ligue 1 na akaposti picha na ujumbe , 'Kwaheri ya mwisho'.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitarajiwa kurejeao Wales kwa wakati kuanza mazoezi asubuhi hii, lakini ndege binafsi ya Piper Malibu aliyopanda ikapoteza mwelekeo na kuanguka karibu na Casquets, Alderney majira ya saa 2.30 usiku wa jana.
Emiliano Sala akikabidhiwa jezi na Mtendaji Mkuu wa Bluebirds, Ken Choo baada ya kukamilihdsa uhamisho wake wa Pauni Milioni 15 kujiunga na Cardiff
Mwenyekiti wa Cardiff City FC, Mehmet Dalman alisema kwamba alikuwa anafuatilia sana taarifa za Sala wakati mchezaji mwenzake wa zamani wa Guingamp, kiungo Lucas Deaux alipotweet: “Natumai kutoka ndani ya moyo wangu kabisa, hii si kweli,”.
Akizungumza kutoka Argentina, baba yake Sala, Horacio alisema alishtushwa na habari hizo juu ya mwanawe, ambaye aliongea naye mara ya mwisho Jumapili.
Dereva huyo wa gari kubwa aina ya lori aliangua kilio huku akimuelezea mwanawe huyo kama 'kijana mdogo jasiri', 'Siwezi kuamini.'
Mama wa mchezaji huyo, Mercedes Taffarel amesema kwamba ndege hiyo mali ya Cardiff City, na Emiliano alikuwa kwenye kipindi kizuri katika maisha yake kwa sasa.
Afisa Mkuu wa kisiwa cha Channel, John Fitzgerald alisema kwamba kuna asilimia tano tu ya kumpata Sala na rubani wake. “Maji yalikuwa baridi mno wakati huo, hivyo kama kulikuwa kuna watu kwenye maji na kwa ubaridi wake wangeweza kudumu kwa saa moja tu kwa majira haya ya mwaka,”alisema.
Ndege ya Piper Malibu iliruka umbali wa futi 2,300 na kupoteza mwelekeo angani kabla ya kuanguka.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2AXrBvb
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms