Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MECHI mbili za Ligi Kuu ya Tanzania Bara za Ndanda FC dhidi ya wenyeji Kagera Sugar iliyokuwa ifanyike kesho Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na dhidi ya Biashara United iliyopangwa kuchezwa Jumatano zimeahirishwa.
Taarifa ya Bodi ya Ligi iliyosainiwa na Mtendaji wake Mkuu, Boniphace Wambura imesema kwamba sababu za kuuahirisha michezo hiyo ni klabu ya Ndanda kupata ajali jana.
Basi la timu ya Ndanda FC liliripotiwa kupata ajali jana wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa safarini kuelekea mkoani Kagera na wachezaji watano Aziz Sibo, Paul Maona, Hemed Khoja, Nassor Saleh na Omar Ramadhan waliripotiwa kupata maumivu madogo madodo.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Barnabas Mwakalukwa alisema jana kwamba ajali hiyo imetokea baada ya gari ya Ndanda kuligonga basi la abiria la Mtei na kusababisha majeraha kwa wachezaji watano wa Ndanda.
Mechi za Ligi Kuu zitaendelea kama kawaida kesho ambazo ni Ruvu Shooting na Azam FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Biashara United na Namungo FC Uwanja wa Karume mjini Musoma na Lipuli FC na Coastal Union Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Aidha, Mwadui FC watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Singida United watawakaribisha mabingwa watetezi, Simba SC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Jumatatu kutakuwa na mechi mbili mjini Mwanza, Uwanja wa Nyamagana Alliance FC dhidi ya Tanzania Prisons na CCM Kirumba ni Mbao FC dhidi ya Mbeya City.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/331KOri
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms