TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2025 baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Zambia ‘Copper Princesses jioni ya leo Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
Bao la Copper Princesses leo limefungwa na Natasha Nkaka dakika ya 53, hivyo wanasonga mbele Raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ushindi wa jumla 4-0 na watakutana na mshindi wa jumla kati ya Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ikumbukwe mechi ya kwanza Serengeti Girls ilifungwa 3-0 na Zambia Jumapili iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam — mabao ya Copper Princesses yakifungwa na Grace Phiri dakika ya 64 na Mercy Chipasula mawili, dakika ya 80 na 89 kwa penalti.
Mwaka jana Serengeti Girs ilitolewa na pia na Copper Princesses katika hatua kama hii ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kuchapwa 5-0 Lusaka Februari 3, kabla ya kushinda 1-0 Dar es Salaam hapo hapo Chamazi Februari 11.
Ikumbukwe Serengeti Girls ni timu pekee ya soka Tanzania iliyowahi kucheza Fainali za Kombe la Dunia – ilikuwa mwaka 2022 nchini India ambako ilifika hadi Robo Fainali na kutolewa na Colombia kwa kuchapwa 3-0.
Katika Kundi lake ilishinda 2-1 dhidi ya Ufaransa, kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Canada kufuatia kufungwa 4-0 na Japan katika mchezo wa kwanza – hivyo kumaliza na pointi nafasi ya pili nyuma ya Japan iliyomaliza na pointi tisa na wote kufuzu Robo Fainali.
Kwa upande wao, Canada walimaliza na pointi mbili ya tatu na Ufaransa waliomaliza na pointi moja wakashika mkia.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/HJhvE6K
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms