• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2025 (281)
    • ►  Desember (33)
    • ►  November (4)
    • ►  September (1)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ►  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ▼  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ▼  November (567)
      • REFA WA TANZANIA APENYA SEMINA YA CHAN 2018 MOROCCO
      • Pro 14: Cheetahs v Scarlets Preview
      • Greyville Friday 1 December 2017 Best Bets
      • Fairview Friday 1 December 2017 Best Bets
      • Ram Slam T20 Challenge: Multiply Titans vs Warrior...
      • Ram Slam T20 Challenge: VKB Knights vs bizhub High...
      • Ram Slam T20 Challenge: Hollywoodbets Dolphins vs ...
      • Sun Met 2018 - Ante Post Betting
      • Van Jaarsveld's return bolsters Dolphins RAM SLAM ...
      • EPL: Arsenal vs Manchester United Preview
      • AZAM TV KUONYESHA MECHI ZOTE 'LIVE' KOMBE LA CECAF...
      • Supersport United Down Ajax
      • Arsene's Gunners Fire Five past Huddersfield
      • Salah Nets Brace off the Bench at Stoke
      • Rooney Revives Everton with Hat-Trick
      • Conte Apologetic after Red Card
      • Guardiola Praises Sterling
      • 17 Transfer Deadline Day Signings
      • MTIBWA SUGAR ‘YAMTIA KITANZI’ BEKI WA SERENGETI BOYS
      • TORRES AFUNGA MAWILI ATLETICO MADRID YAUA 3-0 HISP...
      • BARCELONA YAWAPIGA VIBONDE 5-0 KOMBE LA MFALME
      • RUDIGER AIFUNGIA BAO PEKEE CHELSEA YAIBWAGA SWANSE...
      • SALAH AFUNGA MAWILI LIVERPOOL YACHINJA 3-0 UGENINI
      • RAHEEM STERLING TENA, AIFUNGIA LA USHINDI WA 2-1 M...
      • GIROUD APIGA MBILI, LACAZETTE, SANCHEZ 'MOJA MOJA'...
      • EVERTON YAFUFUA MAKALI, ROONEY APIGA HAT TRICK YAS...
      • MAVUGO MRUNDI PEKEE ANAYECHEZA TANZANIA ALIYEITWA ...
      • KOCHA MPYA EVERTON, ALLARDYCE ASEMA WACHEZAJI HAWA...
      • KIPA WA YANGA, KINDA WA AZAM WAONGEZWA KILI STARS
      • Jerry Sikhosana Calls for Striker Coaches in the PSL
      • HSBC World Sevens Series: Dubai Preview
      • The Ashes: Second Test Preview
      • Kenilworth Thursday 30 November 2017 Best Bets
      • Italian Serie A: Week 15 Preview
      • German Bundesliga: Week 14 Preview
      • Spanish La Liga: Week 14 Preview
      • French Top 14: La Rochelle v Montpellier Preview
      • French Top 14: Toulon v Lyon Preview
      • Top 14: Stade Francais v Racing Metro Preview
      • Alan Pardew Confirmed as West Brom Manager
      • New Zealand vs West Indies: First Test Preview
      • Aviva Premiership: Harlequins v Saracens Preview
      • Telkom Knockout Final: Bidvest Wits v Bloemfontein...
      • Aviva Premiership: Wasps v Leicester Preview
      • Opinion: England need Stokes immediately
      • Manchester United were back amongst the goals as...
      • Wenger Rules out Sanchez and Ozil Departure
      • Mahrez, Vardy Topple Tottenham
      • Scottish Premier League: Week 16 Preview
      • PGA Tour: The Hero World Challenge Preview
      • NINJE APEWA NAFASI YA KUONGEZA WATATU KIKOSI CHA C...
      • CECAFA YACHUKUA MAREFA WAWILI TU TANZANIA
      • HIMID MAO AWASHINDA WAGENI NA KUWA MCHEZAJI BORA W...
      • LEICESTER CITY YAIKANDAMIZA 2-1 TOTTENHAM KING POWER
      • REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE BERNABEU KOMBE LA MF...
      • ASHLEY YOUNG AFUNGA MAWILI, MAN UNITED YAIPIGA 4-2...
      • EUBANK NA GROOVES WATAMBIANA KUELEKEA PAMBANO LAO ...
      • MWANJALI NA MATOLA WALIPOFANYA 'KIKAO CHA DHARULA'...
      • Barrett Wins Back-to-Back World Rugby Player of th...
      • Ram Slam T20 Challenge: bizhub Highveld Lions vs M...
      • Ram Slam T20 Challenge: WSB Cape Cobras vs the War...
      • Stokes Preps for Possible Ashes Call up
      • Messi's Phantom Goal Puts VAR in Motion
      • EPL: Watford v Manchester United Preview
      • Hary Kane All Set for World Cup Debut
      • EPL: Leicester v Tottenham Preview
      • Dortmund Playmaker Ruled out of 2017
      • Marx, Kolisi Return for Boks Final Test
      • SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA JKU UFUNGUZI ‘MAPIND...
      • SIMBA SC WAPEWA SIKU NNE MAPUMZIKO, KUREJEA IJUMAA...
      • BUFFON ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA SERIE A
      • MAN UNITED WAKWEA TRENI KUIFUATA WATFORD, SHUGHULI...
      • SAMATTA AENGULIWA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA
      • AZAM FC 1-1 MTIBWA SUGAR
      • AZAM FC NA MTIBWA SUGAR HAKUNA MBABE, SARE 1-1 CHA...
      • LWANDAMINA AWAPA ‘OFF’ WACHEZAJI WOTE YANGA SIKU SABA
      • BALE AJIFUA REAL MADRID IKIJIANDAA NA KOMBE LA MFA...
      • MAREFA 18 WA TANZANIA WAPEWA BEJI ZA FIFA 2017-2018
      • MWAKYEMBE AWATAKA WACHEZAJI LIGI YA WANAWAKE KUJIT...
      • Vaal Tuesday 28 November 2017 Best Bets
      • SuperSport Scoop R9m, Tinkler Angry at Mazembe Spo...
      • English Premier League Top Players Stats 2017
      • MTIBWA SUGAR: TUMEKUJA DAR KIKAMILIFU KUIVAA AZAM LEO
      • Gattuso Takes over the Reigns at AC Milan
      • OKWI ALIVYOISHUHUDIA SIMBA IKING'ANG'ANIWA NA LIPU...
      • 2017/18 World Sevens Series: Outright Preview
      • Dan Carter Signs for Japanese Rugby Club
      • Messi Pens New 2021 Deal with 700m Euro Buyout Clause
      • NEYMAR NA CAVANI WOTE WAFUNGA PSG YAIPIGA 2-1 MONACO
      • REFA AKATAA BAO LA MESSI, BARCELONA YANG'ANG'ANIWA...
      • SIMBA SC NA LIPULI FC KATIKA PICHA JANA UHURU
      • MSUVAAA….UTAMTAKA! AFUNGA TENA DIFAA EL JADIDA IKI...
      • MSUVAAA….UTAMTAKA! AFUNGA TENA DIFAA EL JADIDA IKI...
      • SIMBA SC 1-1 LIPULI FC
      • MAN CITY YASHINDA MECHI YA 11 MFULULIZO LIGI KUU E...
      • RAIS WA SIMBA 'AKIBURUDIKA' UWANJA WA UHURU LEO...
      • SANCHEZ AFUNGA KWA PENALTI, ARSENAL YASHINDA 1-0
      • NYUSO ZENYE KUASHIRIA KILICHOTOKEA LEO UWANJA WA U...
      • Flamingo Park Monday 27 November 2017 Best Bets
      • SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE NA LIPULI, 1-1 UHURU
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE » SI KILA ANACHOSEMA HAJJI MANARA KIPUUZWE

SI KILA ANACHOSEMA HAJJI MANARA KIPUUZWE

WIKI hii Simba imelalamika kunyimwa penalti mbili na refa Heri Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi ya Oktoba 28, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara pamoja na kuzungumza kwa jazba akiwashutumu mashabiki wa Yanga kufurahia sare hiyo na kuwaponda Waandishi wa Habari na Wachambuzi kwa sababu hawajafanya anavyopenda yeye, lakini alikuwa ana hoja alipozungumzia uchezeshaji wa refa.
Kwa tunayemuelewa Hajji, hatupati naye tabu. Shughuli ya kwanza iliyompatia umaarufu ni siasa akianza kama chipukizi wa CCM, baadaye akaenda Chadema kabla ya kurejea Chama cha Mapinduzi.
Ukweli usiokwepeka, Hajji anatoka ukoo wa soka, baba yake mzazi alicheza Yanga akaenda hadi Ulaya na Amerika. Baba zake wakubwa na wadogo, Kitwana na Kassim nao walicheza Yanga pia. Kassim akaenda kumalizia soka yake Ulaya. Babu yake mzaa mama, Mzee Hajji alikuwa Mwenyekiti wa Simba.  
Lakini yeye Hajji Sunday Manara alianza kuja kwenye michezo miaka ya 2000 kama mwalikwa wa kuchangia mada mbalimbali za kimichezo kwenye vyombo vya Habari, akanogewa naye akaamua kufanya kazi kwenye vyombo vya Habari.
Akaondoka, akarudi kwenye siasa kabla ya Simba kumrejesha kwenye soka kwa kumpa Usemaji wa klabu miaka mitatu iliyopita. Hajji amezoea kulumbana kwenye majukwaa ya siasa, uzoefu ambao anauleta kwenye soka.
Wakati Jerry Muro alipokuwa Msemaji wa Yanga walikutana wote wapenda malumbano na mipasho – wakawa wanapashana haswa. Yanga sasa wana Msemaji mchapakazi, Dissmas Ten asiyependa maneno zaidi ya kazi kwa maslahi ya klabu, Hajji ameamua kulumbana na Waandishi wa Habari na wachambuzi.
Lakini hatupaswi kupuuza kila anachosema tu kwa sababu tumemjua ni mropokaji, bali tumsikilize na kuchukua hoja zake za msingi kuzifanyia kazi, zile pumba zake tumuachie mwenyewe.
Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo huo kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi.
Manara aliyewabeza watani wao hao wa jadi, kwamba ni kawaida yao kupendelewa na marefa kila wanapokutana na Simba amesema watapeleka malalamiko Bodi ya Ligi dhidi ya refa huyo na wengine walioionea timu yao katika mechi zilizotangulia na nakala zimekwenda Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo.
Akasema huo ni mwendelezo wa matukio ya klabu yake kutotendewa haki na marefa katika mechi za Ligi Kuu msimu huu, akidai walinyimwa pia penalti mbili katika mechi dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kabla ya wapinzani wao wengine, Singida United kupewa penalti ya utata Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Simba ilitoa sare ya 2-2 na Mbao FC kabla ya kushinda 3-1 dhidi ya Stand United, katika mchezo ambao pia walikataliwa bao zuri la mshambuliaji wao, Laudit Mavugo.
Hajji aliweka video ambazo zilionyesha kweli wachezaji wa Yanga walinawa mpira, lakini refa Sasii hakufanya chochote.
Rejea  Oktoba 1, mwaka 2016, refa Martin Saanya aliyechezesha mechi ya watani hao wa jadi, alifungiwa miaka miwili kwa pamoja na Msaidizi wake, namba moja, Samuel Mpenzu kwa kuvurunda.
Na pamoja na kuwafungia waamuzi huo kwa makosa ya kutoa maamuzi ya utata, pia Kamati ya Masaa 72 ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilifuta Kadi nyekundu ya mchezaji Jonas Mkude baada ya kubaini hakufanya kosa.
Maamuzi ya utata ya Saanya yalisababisha vurugu Uwanja wa Taifa Jumamosi ya Oktoba 1, mwaka jana baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
Awali, Mpenzu alikataa bao safi la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajib mapema kipindi cha kwanza akidai aliotea.
Mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu baina ya miamba hiyo ulichezeshwa na refa Mathew Akrama kutoka Mwanza Februari 25, mwaka huu pale pale Taifa na winga Shiza Ramadhani Kichuya, kwa mara nyingine aliibuka shujaa wa Simba baada ya kutokea benchi na kuisaidia timu yake kushinda 2-1.
Kichuya aliyempokea beki Novatus Lufunga dakika ya 55, kwanza alimsetia mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuifungia bao la kusawazisha Simba dakika ya 66 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la ushindi dakika ya 81.
Kama Oktoba 1, na Februari 25 Yanga SC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya tano la Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo Mzambia, Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi na Lufunga.
Akrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu beki Mkongo wa Simba, Janvier Besala Bokungu dakika ya 55 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Chirwa.
Akrama alikuwa mwiba kwa timu zote mbili siku hiyo kutokana na maamuzi yake ya kufuata sheria 17 za soka bila kusita pale tu lilipotokea kosa, hali ambayo ilisababisha wachezaji wenyewe waamue kuwa na nidhamu uwanjani.
Na kazi nzuri ya Akrama Oktoba 1 ilikuwa sawa na kusahihisha makosa yake ya Oktoba 3, mwaka 2012 alipochezesha kwa mara ya kwanza mechi ya watani hao wa jadi, ikiwa ya Ligi Kuu pia timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa. 
Katika mchezo huo ulioanza Saa 1:02 usiku, Akrama alimtoa kwa kadi nyekundu winga Simon Msuva wa Yanga dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu beki wa Simba, Juma Nyosso.
Siku hiyo, Simba ndiyo walitangulia kwa bao la kiungo Amri Kiemba dakika ya pili, kabla ya mshambuliaji Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga dakika ya 63 kwa penalti baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira kwenye boksi.
Lakini Akrama alilaumiwa kwa kumuonyesha kadi ya njano badala ya nyekundu kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ licha ya kumchezea rafu mbaya beki wa Yanga, Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul.
Na pia alilaumiwa kuwa kutomchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
Haikuwa ajabu Oktoba 6 Akrama alipoondolewa kwenye orodha ya wamuzi wa kuchezeaha Ligi Kuu baada ya kuvurunda mechi hiyo namba 80, huku aliyekuwa mshika kibendera namba mbili, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam akipewa onyo.
Lakini bado kazi nzuri ya Akrama Februari 25 haiwezi kunibadilisha msimamo wangu wa muda mrefu wa kutaka mechi za watani hawa wa jadi zichezeshwe na marefa wa nje – ila kwa kuwa wenye mamlaka, TFF na Bodi ya Ligi hawajaona umuhimu wa hilo chochote nitakachoandika kitakuwa sawa na kelele za chura, hazitamzuia ng’ombe kunywa maji. 
Lakini ukweli unabaki pale pale, marefa wetu wamesababisha adha kubwa kwenye mechi za watani, achilia mbali za Oktoba 1, mwaka jana kuna matukio mengine makubwa ya kihistoria yamewahi kutokea na kuhatarisha hata maisha ya viongozi wetu wakubwa wa nchi.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi alinusurika katika tukio la hatari Machi 31, mwaka 2002 katika fainali ya Kombe la Tusker, Simba ikishinda 4-1.
Siku hiyo refa Abdulkadir Omar ‘Msomali’ aliivuruga mechi na kuhatarisha amani uwanjani pia kwa madudu yake.
Mechi hiyo ya fainali ambayo Alhaj Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa alikuwa mgeni rasi – chupuchupu  ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka Suleiman kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. 
Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, (FAT), sasa TFF kabla ya kujiuzulu uongozi wa klabu hiyo baadaye.
Ni marefa wachache sana wamewahi kuziongoza vizuri mechi za Simba na Yanga na zikamalizika bila manung’uniko, akiwemo mwanamama mwenye beji ya FIFA, Donisya Rukyaa wa Kagera anayefuata nyayo za marefa wakongwe kama Nassor Hamdoun wa Kigoma.
Tathmini mbalimbali za kitaalamu za vyombo vya habari vya kimataifa zimekwishaipitisha mechi ya Simba na Yanga kama moja ya mechi kubwa mno za watani wa jadi Afrika.
Tatizo kubwa ni marefa, kweli ilipofikia na kama kweli lengo ni kuiongezea msisimko zaidi mechi ya watani, waamuzi wa Tanzania wawekwe kando na watumike waamuzi kutoka nje ya nchi, tena ikibidi nje kabisa ya nchi tatu za Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.
Rejea hata mchezo wa Machi 5, mwaka 2011 Uwanja wa Taifa, refa Orden Mbaga aliivuruga mno mechi hiyo, kutokana tu na pengine mchecheto ama kutaka kufanya kile ambacho kinaitwa ‘kubalansi’ mchezo au kukwepa lawama, matokeo yake akafanya madudu.
Dakika ya 58 Juma Said Nyosso alimkwatua Mzambia Davies Robby Mwape kwenye eneo la hatari akawapa penalti Yanga na kilichofuatia wengi walijua beki huyo wa Simba atatolewa nje kwa kadi nyekundu, badala yake akampa kadi ya njano.
Ngumu kuamini Mbaga, refa mwenye beji ya Shrikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hajui alipaswa kufanya nini kwa Nyosso, lakini kwa sababu ni refa wa nyumbani na aliongoza wapinzani wa jadi katika mechi ya nyumbani, alihofia kumtoa mchezaji kwa kadi nyekundu angeshushiwa lawama nzito. Marefa hufanyiwa fujo na kupigwa na mashabiki, labda alihofia hali hiyo pia.
Dakika ya 73 Simba walipata bao safi la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Mussa Hassan Mgosi, aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Mghana Yaw Berko kufuatia shuti la mpira wa adhabu, lililogonga mwamba wa juu na kudondokea nyavuni kabla ya kuokolewa na mabeki wa Yanga.
Halikuwa bao lenye shaka yoyote, hakukuwa na kuotea wala dosari yoyote, lakini haieleweki kwa nini Mbaga alilikataa bao hilo awali.
Ilikuwa offside au mpira haukutinga nyavuni hadi akalikataa kwanza? Haijulikani, lakini alilikubali baada ya wachezaji wa Simba kumuambia aangalie kwenye TV kubwa iliyopo uwanjani marudio ya tukio lile na baada ya hapo akaenda kujadiliana na msaidizi wake, ndipo akalikubali.
Tujiulize, kusingekuwa na ile TV, Simba wangedhulumiwa bao lao?
Mbaga alichemsha- lakini si Mbaga tu, marefa wengi wa Tanzania waliwahi kutokota kabla yake na nitakumbushia baadhi ya mechi.   
Agosti 18, mwaka 2002 Simba na Yanga zikitoka sare ya 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu, refa Victor Mwandike aliwaacha mashabiki wa Simba midomo wazi kwa kuwapa Yanga penalti ya utata dakika ya 89 na ushei, ambayo Sekilojo Chambua aliitumia vema kuisawazishia bao timu yake, baada ya Simba kutangulia kufunga kupitia kwa Madaraka Suleiman dakika ya 65.
Oktoba 24, mwaka 2007, refa Osman Kazi alikataa mabao matatu yaliyofungwa na Yanga, yote akidai kipa Juma Kaseja alisukumwa na wachezaji wa Yanga, lakini kwa yeyote atakayerudia kuangalia DVD ya mchezo ule, hawezi kuona ukweli wa madai ya Kazi.
Awali ya hapo, Kazi aliwahi kupuliza filimbi ya kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza katika Nusu Fainali ya Kombe la Tusker mwaka 2005 mjini Mwanza, wakati mchezaji wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ amekwishawatoka mabeki wa Simba na anakwenda na mpira mbele yake amebaki Juma Kaseja tu.
Refa ni mwamuzi wa mwisho- lakini kwa wana Yanga walijutia mno tukio lile kwenye mchezo ambao mwishowe walifungwa 2-0, kwa mabao ya kipindi cha pili ya Emmanuel Gabriel na Mussa Mgosi.
Aprili 19, mwaka 2009, Jerry Tegete aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwa mkono na kutengeneza sare ya 2-2, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Refa makini asingeweza kukubali bao lile, hivyo kwa haya yote lazima tukubali marefa wa Tanzania hawawezi tena kuchezesha mechi za watani wa jadi.
Sababu nyingine za marefa wetu kuzishindwa mechi hizo ni hiyo ya mapenzi yao kwa moja ya timu hizo, kitu ambacho Misri wamekiepuka na mechi ya Zamalek na Ahly inachezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi yao.
Nakumbuka refa kutoka Uganda, Dennis Bate aliyechezesha fainali ya mwisho ya Kombe la Tusker mwaka 2009 kati ya Simba na Yanga, aliiongoza vizuri mechi hiyo na akadhibiti ujanja wote wa wachezaji kutaka kumdanganya na hatimaye aboronge.
Kuna wachezaji wanaitwa wazoefu wa mechi za Simba na Yanga na hawa wamekuwa wakiwapoteza sana marefa kwa uzoefu wa kucheza mechi hizo, lakini kama marefa watatoka nje ya Tanzania, tena wa kiwango cha beji za FIFA, uhondo wa mechi za watani utaongezeka maradufu. 
Ndiyo maana ninasema si kila anachosema Hajji Manara ni cha kupuuzwa, kama hili la marefa lifanyiwe kazi.


from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2yvNbHX best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang SI KILA ANACHOSEMA HAJJI MANARA KIPUUZWE. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/11/si-kila-anachosema-hajji-manara-kipuuzwe.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 00.07
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MTANZANIA Alice Gyunda miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha taj...
  • BARCELONA 3-1 ALAVES
    BARCELONA 3-1 ALAVES
    from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2s2Iqyx
  • TUZO ZA LIGI KUU ZABORESHWA, SASA WACHEZAJI KUPEWA NA KING'AMUZI CHA AZAM TV
    Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura, akionyesha tuzo atakayokuwa akipewa Mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vod...
  • ARSENAL YAMUONGEZEA MSHAHARA SANCHEZ ASIENDE BAYERN MUNICH
    KLABU ya Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates. Ofa mp...
  • EPL: Week 36 Preview
    EPL: Week 36 Preview
    We preview week 36 of the 2017/18 English Premier League season which is set to get underway on Saturday 28 April.  We’re into the final s...
  • Woolavington 2000 - Final Field
    View the final field and betting for the Grade 1 Woolavington 2000 at Greyille this Saturday 3 June 2017. The final field for the Woolav...
  • NFD: Week 20 Preview
    NFD: Week 20 Preview
    This will be a tricky week in the GladAfrica Championship with some of the teams having the Nedbank Cup last 32 action in mind. However, I...
  • CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    BAO pekee la beki wa kimataifa wa England, Ben Chilwell dakika ya 45 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford Uwanja wa...
  • Cup Finals Weekend Preview
    We take a look at this weekend's big European Cup Final ties. Most of Europe’s big leagues are done and dusted but there’s still the...
  • YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO
    KLABU ya Yanga imewasimamisha wachezaji wake wawili, Dickson Ambundo na Mrundi Saido Ntibanzokiza kuelekea mechi ya Fainali ya Kombe la S...
Copyright Viral Sports: SI KILA ANACHOSEMA HAJJI MANARA KIPUUZWE