Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Afrika limemteua refa Msaidizi, Frank John Komba wa Tanzania katika orodha ya marefa watakaopata mafunzo ya kuwania kuchezesha Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) inayotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 4 mwakani nchini Morocco.
Komba ni refa msaidizi, maarufu kama mshika kibendera ambaye anakwenda kuwania kuchezesha fainali za pili mfululizo za Afrika, baada ya Mei mwaka huu kwenda Gabon kwenye fainali za U-17 za Afrika.
Marefa wote 44 walioteuliwa wapo mjini Cairo, Misri tangu Novemba 27 hadi Desemba 1 kupata mafunzo maalum ya kuteua marefa wa kuchezesha mechi za fainali hizo zinazotarajiwa kupigwa katika miji ya Casablanca, Marrakech, Tangiers na Agadir.
Frank John Komba (kulia) ni refa pekee wa Tanzania aliyeteuliwa kuchezesha CHAN mwakani
Marefa hao kutoka nchi 35 wanachama wa CAF, wanawania nafasi ya kuchezesha fainali za tano za CHAN zinazokutanisha wachezaji wanaocheza kwenye ligi za nchini mwao pekee na mafunzo yao ni ya nadharia na vitendo.
Mafunzo mapya kwao yatakuwa ni matumizi ya Teknolojia ya picha za Video (VAR) kutoa maamuzi, mfumo ambao utafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya CHAN mwakani.
Meneja wa Marefa wa CAF, Eddy Maillet amesema kwamba marefa watakaochezesha fainali za Total CHAN Morocco 2018 watatajwa siku tano baada ya kozi hiyo.
Kundi A linaundwa na wenyeji, Morocco, Guinea, Sudan na Mauritania, Kundi B kuna Ivory Coast, Zambia, Uganda na Namibia, Kundi C linaundwa na Libya, Nigeria, Rwanda na Equatorial Guinea na Kundi D lina timu za Angola, Cameroon, Kongo na Burkina Faso.
Mechi ya ufunguzi na fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Mohamed V Complex mjini Casablanca, ambao pia ulitumika kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2017.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2i5DHZ2
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang REFA WA TANZANIA APENYA SEMINA YA CHAN 2018 MOROCCO. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/11/refa-wa-tanzania-apenya-semina-ya-chan.html. Terimakasih atas perhatiannya.