Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
SIMBA SC wameshindwa kuutumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Sare hiyo inamaanisha Simba SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 22 baada ya mechi 11, ikiwazidi kwa pointi mbili tu mabingwa watetezi, Yanga ambao nao jana walilazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, aliyesaidiwa na Khalfan Sika wa Pwani na Vincent Mlabu wa Morogoro iliwachukua dakika 15 tu Simba kupata bao la kuongoza, lililofungwa na kiungo wake mkongwe, Mwinyi Kazimoto Mwitula.
Kazimoto alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya kiungo mwenzake, Muzamil Yassin mbele ya mstari wa kuugawa Uwanja na kutembea nayo hatua mbili kabla ya kumtungua kwa mpira wa juu kipa wa Lipuli, Agathony Mkwando aliyetokea kujaribu kuokoa.
Simba ilipata bao hilo ikitoka kupoteza nafasi tatu nzuri za kufunga mabao kupitia kwa nyota wake John Bocco, Shiza Kichuya na Muzamil Yassin.
Lipuli walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika nne baadaye kupitia kwa Nahodha wao, Mghana Asante Kwasi aliyefunga kwa shuti la mpira wa adhabu.
Baada ya baio hilo, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini ni ndiyo waliotengenewza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.
Kipindi cha pili, Simba SC waliendelea kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Lipuli, lakini wakashindwa kutumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza.
Safu ya ulinzi ya Lipuli ikiongozwa na mabeki wa zamani wa Simba SC, Novaty Lufunga na Mganda Joseph Owino ilijitahidi kutibua mipango mingi ya safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussen ‘Tshabalala’, James Kotei,
Yusuph Mlipili, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Haruna Niyonzima.
Lipuli FC; Agathony Mkwando, Asante Kwasi, Hussein Rashid, Ally Mtoni, Joseph Owino, Hamad Manzi/Novaty Lufunga dk35, Seif Rashid, Mussa Nampaka, Ramadhani Mandebe, Malimi Busungu na Shaaban Ada.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2Abcqgj
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE NA LIPULI, 1-1 UHURU. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/11/simba-sc-yalazimishwa-sare-na-lipuli-1.html. Terimakasih atas perhatiannya.