Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa klabu kwa mwezi Oktoba baada ya kuwashinda wageni watatu, Waghana kipa Razak Abalora, beki Yakubu Mohammed na Mzimbabwe beki Bruce Kangwa pamoja na mzalendo mwenzake, Aggrey Morris.
Mao anakuwa mchezaji wa tatu msimu huu kushinda tuzo hiyo baada ya Yakubu Mohammed aliyeshinda Agosti na mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyeibeba Septemba.
Nahodha huyo msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ametwaa tuzo hiyo baada ya kujizolea kura 320 za mashabiki zikiwa ni asilimia 47 ya kura zote 680 zilizopigwa kupitia mtandao wa poll kwenye akaunti ya facebook ya Azam FC.
Himid Mao ‘Ninja’, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Azam FC mwezi Oktoba
Aidha kipa mahiri wa timu hiyo, Razak Abalora, ambaye mpaka sasa amefungwa mabao matatu kwenye mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ameshika nafasi ya pili baada ya kujizolea kura 292 sawa na asilimia 43 za kura zote zilizopigwa.
Beki wa kushoto, Kangwa ameshika nafasi ya nne kwa kura 41 alizojizolea (asilimia sita) huku Moris akimalizia orodha hiyo baada ya kukusanya kura 27 zikiwa ni asilimia nne za kura zote zilizopigwa na mashabiki (680).
Tuzo hiyo inadhaminiwa na Wadhamini wakuu wa Azam FC, Benki ya NMB, ambayo kwa sasa ndio bora kabisa Tanzania ikikuhakikishia usalama wa fedha zako na ikiwa na matawi mengi yaliyosambaa kote hapa nchini.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2BvIg7K
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms