Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MTIBWA Sugar inaondoka kesho Manungu mkoani Morogoro kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Jumamosi Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Lakini katika msafara huo, Mtibwa Sugar haitakuwa na wachezaji wake watatu majeruhi, kipa Shaaban Kado, beki Salum Kanoni na kiungo Haroun Chanongo.
Katibu Msaidizi wa timu, Abubakar Maswabur amesema kwamba wachezaji hao watatu wanaendelea na matibabu na wanatarajiwa kurejea katikati ya mwezi huu.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaondoka kesho Manungu kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo na Ndanda FC
Maswabur amesema wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa wanajivunia kutowahi kufungwa na Ndanda popote tangu timu hiyo ya Mtwara ilipopanda Ligi Kuu mwaka 2014. Katika michezo sita ambayo timu hizo zilikutana, Mtibwa wameshinda mara nne na mingine miwili wametoka sare. Mtibwa Sugar wamefunga jumla ya mabao 10 katika mechi hizo, huku Ndanda wakifunga mabao manne.
Kwa ujumla, Ligi Kuu itaendelea Ijumaa, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Jumamosi Singida watakuwa wenyeji wa Yanga Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda.
Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili kutakuwa na mechi mbili, mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2h2dVs0
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang MTIBWA SUGAR WAJIVUNIA REKODI YA KUTOFUNGWA NA NDANDA FC. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/11/mtibwa-sugar-wajivunia-rekodi-ya.html. Terimakasih atas perhatiannya.