
KLABU ya Real Madrid ya Hispania imesajili beki wa Kimataifa wa England, Trent John Alexander-Arnold (26) ambaye hucheza nafasi ya kiungo pia kwa mkataba wa miaka sita kutoka Liverpool ya England kwa ada ya Dola za Kimarekani Milioni 11.3.
Taarifa ya Real Madrid imesema kwamba wamefikia makubaliano na Liverpool FC kumsajili Trent kwa miaka sita kuanzia Juni 1 June mwaka huu, 2025 hadi Juni 30 mwaka 2031.
Trent Alexander-Arnold anakwenda kuungana na mchezaji mwenzake wa England, kiungo Jude Victor William Bellingham (21) aliyesajiliwa Real Madrid Juni 14 mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka sita pia kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani aliyojiunga nayo mwaka 2020 akitokea Birmingham City ya nyumbani.
Kisoka Alexander-Arnold aliibukia katika akademi ya Liverpool aliyojiunga nayo mwaka 2004 na alikuwa Nahodha wa timu za vijana. Alianza kuchezea timu ya wakubwa msimu wa mwaka 2016 akiwa ana umri wa miaka 18 na akacheza mfululizo Fainali za Ligi ya Mabingwa msimu wa 2018 na 2019, akishinda baadaye na kuchaguliwa kwenye kikosi Bora cha Ligi ya Mabingwa msimu huo.
Kucheza huko mfululizo kulimfanya aweke rekodi ya mchezaji mdogo zaidi kuwahi kutokea aliyecheza Fainali zilizofuatana za michuano hiyo.
Mwaka huo huo, alitwaa mataji ya UEFA Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA, wakati katika mashindano ya nyumbani Alexander-Arnold alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa msimu wa the 2019–20 sambamba na Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu England.
Sambamba na kuingia kwenye Kikosi Bora cha msimu cha PFA Ligi Kuu ya England na kuiwezesha Liverpool kutwaa taji la 30 la Ligi Kuu ya England msimu wa 2019–20.
Mafanikio yake mwaka 2020 yalimfanya achaguliwe kwenye kikosi cha Wachezaji 11 Bora cha FIFA FIFPRO Wanaume, wakati msimu wa 2021–22 alitwaa mataji mawili ya nyumbani ambayo ni Kombe la Ligi na Kombe la FA.
Alexander-Arnold ameichezea timu ya England kuanzia timu za vijana, kabla ya kuanza kuchezea timu ya wakubwa mwaka 2008 na yangu wakati huo amecheza Kombe la Dunia mwaka 2018 ambako aliweka rekodi ya mchezaji wa nne mdogo zaidi kuanza kwenye kikosi cha England kwenye michuano ya UEFA Nations League ambako walishika nafasi ya tatu.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG https://ift.tt/qCQpuse
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang REAL MADRID YAMSAJILI TRENT ALEXANDER-ARNOLD MIAKA SITA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2025/05/real-madrid-yamsajili-trent-alexander.html. Terimakasih atas perhatiannya.