
TIMU ya soka ya taifa Tanzania inatarajiwa kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) inayotarajiwa kuanza Juni 4 Uwanja wa Free State Toyota mjini Bloemfontein nchini Afrika Kusini.
Kocha Hemed Morocco atataja kikosi cha Taifa Stars wakati wowote ambacho kitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya michuano hiyo – lakini wataanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Bafana Bafana Juni 6 kuanzia Saa 2:30 usiku Uwanja wa Peter Mokaba Jijini Polokwane, Pietersburg.
Kwenye Kombe la COSAFA Tanzania imeorodheshwa dakika za mwisho baada ya Morocco kujitoa na imepangwa Kundi C pamoja na Ewatini na Madagascar, wakati Kundi A wapo wenyeji Afrika Kusini, Mauritius, Msumbiji na Zimbabwe na Kundi B linazikutanisha Angola, Lesotho, Malawi na Namibia.
Taifa Stars itacheza mechi yake ya kwanza ya COSAFA Juni 7 dhidi ya Madagascar kabla ya kumalizia na Eswatini Juni 11 kuagalia mustakabali wake wa kwenda Nusu Fanali ambazo zitafuatia Juni 13 na Fainali ni Juni 13 sambamba na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Mara ya mwisho Tanzania ilishiriki michuano ya COSAFA mwaka 2017 Jijini Rusternburg nchini Afrika Kusini na kutolewa katika hatua ya Nusu Fainali ikifungwa mabao 4-2 na Zambia Julai 5, mabao ya Taifa Stars yakifngwa na Erasto Nyoni dakika ya 16 na Simon Msuva dakika ya 85, huku ya Chipolopolo yakifungwa na Brian Mwila dakika ya 44, Justin Shonga mawili dakika ya 45+2' na 68 na Jackson Chirwa kwa Penalti dakika ya 56.
Taifa Stars ilianza vyema kwa kuongoza Kundi A mbele ya Angola, Mauritius na Malawi ikivuna ponti tano na kuizidi tu wastani wa mabao Angola, huku Mauritiusn na Malawi kila moja ikiambulia pointi mbili.
Taifa Stars ambayo mechi zake za Kundi A iliifunga Malawi 2-0 na kutoa sare ya 0-0 na Angola na 1-1 na Mauritius – kwenye Robo Fanali iliwatoa wenyeji, Bafana Bafana bao pekee la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 18.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG https://ift.tt/P0Yf5B3
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang TAIFA STARS KUSHIRIKI KOMBE LA COSAFA AFRIKA KUSINI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2025/05/taifa-stars-kushiriki-kombe-la-cosafa.html. Terimakasih atas perhatiannya.