 |
Mnenge Suluja wakati anacheza
Toto Africans mwaka 1995 |
WINGA machachari wa zamani wa Simba SC, Mnenge Suluja Junior amefariki Dunia usiku wa jana mkoani Geita.
Kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba SC, Athumani Chama marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo.
Chama amesema umauti umemkuta nyumbani kwake, Geita siku nne baada ya kurejea kutoka Mwanza ambako alikuwa amelazwa kwa wiki moja kwa matibabu hospitali ya Bugando.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho mchana kwenda nyumbani kwa marehemu, Sengerema.
Hadi umauti unamkuta, Suluja ambaye kisoka aliibukia Pamba ya Mwanza kabla ya kusajiliwa Simba SC mwaka 1997 — alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Geita (GEDFA).
Mbali na Pamba na Simba SC, Mnenge pia alichezea timu za Kariakoo United ya Lindi na Pallson ya Arusha pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akianzia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Vijana Stars, sasa Ngorongoro Heroes.
Mzaliwa huyo wa Buzuruga, Mwanza ambako aliibukia kisoka, kabla ya Pamba alicheza timu za AFC Lumumba na Toto Africans za Jijini humo.
Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.
Mnenge Suluja (kushoto) akiwa na Wyclif Ketto (katikati) Said Maulid 'SMG' (kulia) wakati wanacheza Simba SC mwaka 2000
Mnenge Suluja wa pili kutoka kushoto walioketi katika kikosi cha Pamba SC mwaka 1997
Mnenge Suluja wa tatu kutoka kushoto waliopiga magoti akiwa na kikosi cha AFC Lumumba mwaka 1995
Mnenge Suluja wa sita kutoka kulia waliosimama akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 1999
from BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE https://ift.tt/9p8AawE
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms