
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amezipongeza timu ya taifa Futsal na ya vijana chini ya miaka 15 kwa kufanya vyema kwenye mashindano ya Kimataifa.
“Ninaipongeza Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 15 kwa kuwa mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Shule za Afrika (CAF African Schools Football Championship) kwa mara ya pili mfululizo. Ninajivunia ushindi wenu kwani ni fahari kwa Taifa letu na chachu ya kuendelea kukua kwa sekta ya michezo nchini,” amesema Rais Dk. Samia katika taarifa yake leo.
Tanzania juzi ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Shule za Afrika (ASFC), inayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 15 kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa Penalti 3-2 dhidi ya Senegal kufuatiua sare ya bila mabao Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ghana Jijini Accra.
Hiyo inakuwa mara ya pili mfululizo kwa vijana hao wa Tanzania kutwaa taji hilo baada ya mwaka jana pia kuwa mabingwa visiwani Zanzibar.
Upande wa wanawake, wenyeji Ghana waliweka heshima baada ya kutwaa ubingwa kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uganda.

Aidha, Rais Samia ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal kwa kuingia Fainali ya mashindano ya Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.
“Hongereni wanangu Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mchezo wa Futsal kwa kufuzu kuingia fainali ya mashindano hayo kwa Bara la Afrika, na wakati huo huo kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Dunia la Futsal kwa Wanawake 2025 ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), yatakayofanyika huko Manila, Ufilipino baadaye mwaka huu,” amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kuongoza;
“Nimefurahishwa na juhudi na nidhamu yenu katika mashindano haya. Ushindi wenu ni heshima kwa nchi yetu, na hamasa zaidi kwa watoto wa kike kushiriki katika michezo, si tu kwa burudani lakini pia kama ajira. Ninawapenda na ninawatakia kila la kheri,”.
Tanzania imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya Futsal kwa Wanawake Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cameroon leo Uwanja wa Salle Moulay Abdellah Jijini Rabat nchini Morocco inakofanyika michuano hiyo.
Mabao ya Tanzania yamefungwa na Vaileth Nicholas dakika ya 31, Aisha Mnunka dakika ya 35 na Anastazia Katunzi dakika ya 38, wakati ya Cameroon yamefungwa na Pekure dakika ya 32 na Beulou dakika ya 36.
Tanzania sasa itakutana na wenyeji Morocco, ambao wameitoa Angola kwa kuwachapa mabao 5-1 usiku huu hapo hapo Uwanja wa Salle Moulay Abdellah.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/tZelnsA
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang RAIS SAMIA AZIPONGEZA TIMU ZA TAIFA ZA FUTSAL NA WANAFUNZI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2025/04/rais-samia-azipongeza-timu-za-taifa-za.html. Terimakasih atas perhatiannya.