FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazoendelea nchini Morocco zimeguswa na habari za kusikitisha za kifo cha mtoto wa nyota wa zamani wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki.
Nyota huyo wa Burkina Faso kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kimataifa na nchi yake kwenye mashindano hayo huku timu yake ikitoa heshima kwa habari hizo za kuhuzunisha.
Taarifa inasomeka: "Kwa masikitiko na huzuni kubwa, Wydad AC inatoa rambirambi zake za dhati kwa mchezaji wetu Aziz Ki kwa kifo cha mtoto wake.
"Tunamwomba Mwenyezi Mungu amrehemu marehemu, ampumzishe mahali pema peponi, na awape familia yake na wapendwa wake uvumilivu na faraja."
Katika usiku wa Mwaka Mpya, Aziz Ki aliisaidia nchi yake kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye Kundi lao, E na kufuzu Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi dhidi ya Sudan.
Siku huyo, Aziz Ki alitoa pasi ya kupatikana bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 ambao ulihakikisha nafasi ya pili.
Wanakabiliwa na mtihani mkubwa katika hatua ya 16 Bora dhidi ya Ivory Coast huku mchezo huo ukifanyika Jumanne, Januari 6.
Aziz na wenzake walishinda michezo miwili na kupoteza mmoja katika Kundi E.
Walishinda 2-1 dhid ya Equatorial Guinea, kabla ya kupoteza 1-0 mbele ya Algeria waliooongoza Kundi.
Ushindi dhidi ya Sudan kisha ukahakikisha nafasi ya pili kwa gharama ya Sudan huku timu hizo mbili zikiwa sawa kwa pointi kabla ya pambano hilo.
Aziz Ki, mwenye umri wa miaka 29, anachezea klabu ya Wydad Athletic ya Morocco aliyojiunga mwaka jana akitokea Young Africans ‘Yanga SC’ ya Tanzania.
from BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE https://ift.tt/L5TQgti
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms